Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 14 Machi 2015 10:49

Mauaji ya Kimbari (21) MWISHO

Mauaji ya Kimbari (21) MWISHO

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Karibuni wasikilizaji wapenzi katika sehemu hii ya 21 ya mfululizo wa makala hizi fupi fupi za mauaji ya kimbari katika zama zetu hizi. Tunataraji kuwa hii itakuwa ni semehu ya mwisho ya mfululizo huu, licha ya kwamba bado kuna mambo mengi sana yanapaswa kuzungumzwa kuhusiana na mada hii, kwani kila leo kunaripotiwa mauaji mapya ya kimbari huku mkono wa madola ya kibeberu ukionekana waziwazi kwenye jinai hizo.


*******


Wapenzi wasikilizaji, katika sehemu iliyopita tuliahidi kuendelea kugusia mauaji ya kimbari na jinai zinazofanywa na makundi ya kigaidi ya nchini Syria na Iraq dhidi ya watu wasio na hatia wakiwe wasio Waislamu, huku madola ya kibeberu yakikiri kwamba ndiyo yaliyounda makundi hayo ya kigaidi. Tumeshazungumza kwa muda kidogo jinai zinazofanywa na makundi hayo ya kigaidi dhidi ya wananchi ambao kwa asilimia kubwa ni Waislamu huko Iraq na Syria. Siku chache zilizopita, yaani mwanzoni mwa mwezi huu wa Machi, Wakristo wa Kiassyria wa Iraq na Syria walifanya maandamano katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kutangaza kuwa kwao pamoja na Wakristo wenzao 220 waliotekwa nyara na kundi la kigaidi la Daesh huko Syria. Wakristo hao walibeba mabango kulaani misimamo ya makundi ya kigaidi ambayo yanamkufurisha kila asiyekubaliana na fikra zao. Kabla ya hapo pia, kundi la Daesh liliushitua ulimwengu kwa kuwashambulia na kigaidi Wakristo na watu wa kabila la Izadi au kwa jina jingine Yazidi huko kaskazini mwa Iraq, na kunajisi wanawake na wasichana pamoja na kuchinja watu hadharani kama silaha ya kueneza hofu. Cha kutisha zaidi ni kuwa, kila jinai inayofanywa na Daesh inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii, na kuoneshwa katika kila kona ya dunia. Magaidi hao ni matunda ya siasa za kibeberu za madola ya Magharibi. Hata wakati kundi la Daeshi lilipouvamia mkoa wa Salahuddin huko Iraq, makumi ya maelfu ya watu wa kabila la Izadi walikimbilia milimani, huku baadhi ya taasisi za kimataifa zikitangaza hatari ya kutokea mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa kabila hilo. Gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza liliwahi kuandika kuwa, zaidi ya mateka 500 wa kabila la Yazidi walizikwa wakiwa hai na genge la mauaji la Desh huku karibu watoto 40 wa Izadi wakiwa miongoni mwa waliokumbwa na mauaji hayo. Picha zilizoenezwa mitandaoni na genge la propaganda la Daesh zinazonesha kwa uwazi balaa kubwa sana iliyowakumba watu wa kabila hilo. Picha hizo zilizonesha jinsi wanamgambo wa Daesh walivyowasimamisha katika mstari wanaume wa kabila hilo, na baadaye kuwaua kwa umati. Akitoa hotuba katika bunge la Iraq, Bi Vian Dakhil, mbunge wa watu wa kabila la Yazidi nchini Iraq alisema, hadi wakati anatoa ripoti hiyo, wanaume 500 wa kabila la Izadi walikuwa wameshauliwa kwa umati, wanawake kunajisiwa, watoto wengi kuuwa na wanawake wengine wengi kufanywa mateka na masuria waliouzwa kama bidhaa. Kamanda mmoja wa kundi la kigaidi la Daesh naye alithibitisha jambo hilo wakati alipohojiwa na televisheni ya Marekani ya CNN na kusema kuwa wasichana wa Izadi waligaiwa wanamgambo wa Daesh kuwa mali yao na kuingizwa kwa nguvu katika ufuska wa kijinsia uliopewa jina la Jihadun Nikah. Alikiri pia kuwa wanawake na watoto mia moja wa kabila la Izadi walitekwa huko Sanjar Iraq na kupelekewa Mosul, huku idadi kubwa kati yao wakiuliwa kwa umati. Jinai zote hizo zinafanywa na kundi la kigaidi la Daesh ambalo madola ya kibeberu hususan Marekani hayaoni hata soni kutangaza mbele ya kamera za ulimwengu kwamba wao ndio walioliunda kundi hilo. Muda umetuishia ingawa bado kuna mengi yamebakia.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

 

Zaidi katika kategoria hii: « Mauaji ya Kimbari (20)

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)