Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 24 Januari 2015 11:06

Mauaji ya Kimbari (15)

Mauaji ya Kimbari (15)

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Hii wapenzi wasikilizaji ni sehemu ya 15 ya makala za Mauaji ya Kimbari katika zama zetu hizi. Katika sehemu iliyopita na wakati tulipojadili jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashambulizi yake ya siku 50 huko Ghaza, tulisema kuwa mauaji hayo ya kimbari yalikuwa makubwa kiasi kwamba hata zaidi ya Mayahudi 300 walionusurika kwenye mauaji ya Mayahudi wakati wa utawala wa Hitler nchini Ujerumani au wana na wajukuu wa wahanga hao waliandika barua ya wazi kulaani mauaji ya kimbari ya Israel huko Ghaza. Barua hiyo ilichapishwa kwenye gazeti la New York Times toleo la Jumamosi, Agosti 23, 2014 na waliotia saini barua hiyo ya wazi waliitaka Israel iache kuuzingira Ukanda wa Ghaza na waliilaumu pia Marekani kwa kuchochea mauaji hayo kutokana na misaada yake ya kila namna kwa utawala wa Kizayuni. Barua hiyo ilibeba kichwa kisemacho: Mauaji ya Kimbari mbele ya kimya cha walimwengu. Leo tutaendelea na tulipofikia. Karibuni.
KASIDA
Wakati dunia nzima ilishuhudia maandamano ya watu wa kila rika kulaani jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza, jambo la kusikitisha lilikuwa ni kwamba taasisi za kimataifa na hususan Baraza la Usalama la Umoja wa Marekani lilishindwa kutekeleza wajibu wake na halikuwazuia Wazayuni kutenda mauaji ya kimbari huko Ghaza. Utawala wa Kizayuni ulikanyaga vibaya sheria za kimataifa na haki za binadamu katika Ukanda wa Ghaza, lakini Umoja wa Mataifa na taasisi zinazojinadi kutetea haki za binadamu zilionesha wazi kuwa zinaposema mwanadamu hazikusudii taifa la Palestina. Kwani si tu kwamba, mauaji ya kimbari na uangamizaji wa kizazi uliofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza uliungwa mkono na viongozi wa Marekani tu, lakini ukimya wa kutisha uliooneshwa na taasisi zenye ushawishi duniani nao ulipiga muhuri wa kutilia nguvu jinai za Israel huko Ghaza.
Alaakullihaal, huo ulikuwa ni upande mmoja wa sarafu ya kadhia ya Ghaza uliojaa majonzi, biwi la simanzi na kite pamoja na kukanyagwa misingi yote ya kibidanamu, kisheria na mauaji ya kikatili dhidi ya watu hasa watoto wadogo na wanawake wasio na hatia, lakini upande wa pili wa sarafu ya matukio ya Ghaza nao ulikuwa na matukio ya aina yake. Hasira za walimwengu dhidi ya utawala wa Kizayuni ambao siku zote ulikuwa unajifanya umedhulumiwa, ziliongezeka sana. Kwa jinai zake hizo, Israel ilimuonyesha kila mwanadamu kuwa ni utawala katili usio na chembe ya utu na ubinadamu. Watu wote wanaopigani ukombozi, amani na usalama, Waislamu wa kila rika, wapinzani wote wa vita, ugaidi na utumiaji mabavu, wapinzani wote wa udikteta wa kisiasa usio na huruma, watetezi wote wa sheria za kimataifa, wote kwa ujumla wao walikuwa na kauli moja katika kupinga na kulaani jinai hizo za Wazayuni bila ya kujali tofauti zao za kitaifa, kidini na kizazi. Wote waliyakinikiwa kwamba, Israel ni tishio kwa usalama wa dunia na kwamba kuwepo kwake hakuendani na kuwepo usalama na utulivu duniani. Kwa miaka mingi utawala huo unaoukalia kwa mabavu mji mtakatifu wa Quds na waungaji mkono wake wamekuwa wakitekeleza siasa za kikatili dhidi ya wananchi wa Palestina na hawakubakisha fursa yoyote ya kupatikana amani.
Wapenzi wasikilizaji, muda wa sehemu hii ya 15 ya mfululizo wa makala hizi za Mauaji ya Kimbari katika zama zetu hizi umeisha. Tukutane kwenye kipindi kijacho tukijaaliwa. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

 

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)