Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 10 Januari 2015 09:06

Mauaji ya Kimbari (13)

Mauaji ya Kimbari (13)

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Hii ni sehemu ya 13 ya mfululizo huu wa makala zinazozungumzia mauaji ya kimbari katika zama zetu hizi. Katika sehemu ya 12 ya mfululizo huu tulianza kutupia jicho mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi waliozingirwa kila upande wa Ukanda wa Ghaza. Mauaji hayo ya kimbari ni yale yaliyofanywa na Israel katika mwezi wa Ramadhani yaani takriban miezi saba iliyopita. Tulisema katika sehemu moja ya makala hiyo kwamba, ilionekana wazi kuwa Wazayuni walikuwa na chuki za muda mrefu dhidi ya binadamu, dhidi ya hospitali na vituo vya matibabu, dhidi ya magari ya wagonjwa na ya misaada, dhidi ya misikiti na mashule, dhidi ya raia, dhidi ya miti, dhidi ya wanyama na dhidi ya kila kitu kilichoonekana kwenye Ukanda wa Ghaza. Walikuwa wanashambulia kwa hamaki na chuki, kila kilichokuwa mbele yao na hasa watoto. Leo tutaendelea na tulipofikia. Karibuni.
                                                                                                          *******
Visa vya kuuliwa watoto katika mashambulizi ya siku 50 ya Wazayuni huko Ghaza vyenyewe vina uwanja mpana wa kuzungumziwa. Walimwengu walikuwa wakiona kwenye vyombo vya habari namna wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walivyokuwa wanawaua kwa umati na kikatili watoto wadogo. Picha na video nyingi zinaonesha wazazi wa watoto hao wakiwa wameinyanyua juu miili ya vitoto vyao huku wakilia kwa uchungu wakisema, watoto hawa wameuliwa kwa kosa gani? Ukatili wa wanajeshi wa Kizayuni ni mkubwa kiasi kwamba, wakati watoto walipokuwa wanauwa kwa umati huko Ghaza, katika maeneo ya kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, Wazayuni walikuwa wakisherehekea mauaji hayo na wakitamba kuwa sasa shule za Ghaza hazitakuwa tena na watoto wa kuwasomesha. Mwanajeshi mmoja Mzayuni wa kikosi cha wadunguzi yaani wanaodungua watu kwa risasi kutokea mbali, alijifakharisha katika ukurasa wake wa Twitter kwa kusema kuwa amewaua kwa kuwadungua kwa mbali, watoto 13 wa Palestina. Ripoti nyingine zinaonesha kuwa askari wadunguaji wa Kizayuni walikuwa wanawalenga vichwani moja kwa moja watoto wa Kipalestina katika mauji hayo ya siku 50.
Tab'ani watu wengi duniani wamepata yakini kwamba Wazayuni walikuwa wanafanya mauaji hayo kwa malengo maalumu. Kwa kweli kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina ndilo lililokuwa lengo kuu la Wazayuni katika mauaji hayo ya siku 50. Vyombo vya habari vya Kizayuni vilikuwa vikitangaza hadharani na bila ya kificho kwamba, ilikuwa inajuzu wakati huo kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wa Ghaza. Hivi karibuni gazeti la Kizayuni la Times of Israel liliandika makala maalumu chini ya kichwa cha maneno: Wakati mauaji ya kimbari yalipokuwa yanajuzu. Yochanan Gordon mmoja wa waandishi wa gazeti hilo aliwahi kusema kuwa kuuliwa Wapalestina wote ni jambo linalojuzu. Katika sehemu moja ya makala hiyo mwandishi Mzayuni alisema: Kama viongozi wa kisiasa na wataalamu wa kijeshi watasema kuwa njia pekee ya kuweza kupatikana utulivu wa kudumu ni kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, je itakuwa haijuzu kufanya mauaji hayo kwa watu wanaohisi wajibu wa kutekeleza vizuri majukumu yao? Makala hiyo kwa kweli ilikuwa ni muhuri wa kutilia nguvu malengo ya viongozi wa Israel katika mauaji yao ya kimbari ya siku 50 huko Ghaza.
Amma kichekesho kikubwa cha kihistoria kinajitokeza pale tunapozingatia kwamba wanadamu wangali wanaikumbuka vizuri Ujerumani ya Kinazi ya utawala wa Hitler ya miaka ya 1939 hadi 1945. Msimamo huo wa Wazayuni ndio huo huo aliokuwa nao Hitler, yaani kupenda kutanua mipaka yake ya utawala wa kuzivamia na kuzikalia kwa mabavu nchi nyingine za Ulaya....

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)