Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 15 Januari 2012 12:16

Ulevi, Madhara na athari zake (7)

Ulevi, Madhara na athari zake (7)

Kama tulivyosema ni kuwa, hii leo muundo wa familia unakabiliwa na vitisho na hataritofauti. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa, watu wana nafasi muhimu katika kuundika familia na kuimarisha misingi ya familia na jamii kwa ujumla. Aidha miamala mizuri ya watu ina nafasi muhimu katika kulinda na kuhifadhi misingi ya familia. Hapana shaka kuwa, kama mazingira ya familia hayatokuwa salama, kutakuwa kumeandaliwa uwanja mkubwa kwa ajili ya mambo mabaya likiwemo suala la watoto na vijana wadogo kukimbia na kutoroka nyumbani na kuanza kurandaranda huku na huko. Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuyabadilisha mazingira ya familia iliyojaa, mapenzi, huba na hali ya upendo na kuwa anga ya mivutano, mifarakano na hitilafu. Moja ya sababu hizo ni wanafamilia hususan baba au mama kuwa walevi. Kujihusisha na ulevi mbali na kuhatarisha usalama wa kiuchumi wa familia hupeleke kutokea matatizo mengi kuhusiana na mahusiano ya wanafamilia. Moja ya kazi muhimu ambazo zinapaswa kufanyika kwa ajili ya kuimarisha nguzo ya familia, ni himaya ya kimaisha, kimapenzi na kiakhlaqi katika familia hususan kwa wanawake, watoto na watu wazima. Akina baba ambao wanakunywa pombe, kutokana na kung'ang'ania kutumia ulevi huhisi kutokuwa na uwezo wa kuwatunza wake zao na watoto wao. Suala hilo hupeleke watoto hao kukosa mapenzi ya baba zao. Hali hii hupelekea kutokea hali ya maradhi ya kinafsi na kisaikolojia kwa watoto, sambamba na mashinikizo ya kijamii juu yao. Hii hutokana na kuwa watoto hao hujihisi kuwa hawana watu wa kuwakingia kifua na hawana mtu wa kuwa pamoja nao katika medani mbalimbali za kijamii.
Katika familia mama na watoto ndio ambao huwa wahanga wakuu wa baba mlevi ndani ya familia hiyo. Kupigwa, kutukanwa na miamala mibaya ya mume sambamba na dhana mbaya kwa mkewe ni miongoni tu mwa mambo ambayo humuandama mama ndani ya familia kutoka kwa mumewe ambaye ni mlevi. Vitendo vibaya na miamala ya utumiaji mabavu ya mume mlevi ndani ya familia humharibu kisaikolojia mkewe na kumfanya akate tamaa ya kutekeleza jukumu lake ndani ya familia kama mama. Katika mazingira kama hayo, mama huyo huwa na machaguo mawili: mosi hulazimika kukimbia na kurejea kwao. Pili hulazimika kustahamili vitendo vibaya vinavyotokana na utumiaji ulevi vya mumewe. Mke wa namna hii kutokana na mumewe kughiriki katika ulevi, hulazimika kuchukua jukumu la kulea familia na hata kudhamini mahitaji ya familia yake. Hii hutokana na kuwa, wakati mwingine mume huyo hupoteza hata kazi na ajira aliyonayo kutokana na kutumbukia katika ulevi. Wazazi ambao ni walevi hushindwa kutekeleza ipasvyo majukumu yao ya kifamilia hasa suala la kuwa karibu na watoto na kusimamia nyendo na miamala yao. Kwa msingi huo watoto huanza kujifanyia mambo watakayo pasina ya kuweko wa kuwakanya na kuwaongoza. Watoto wa wazazi mbao wanakunywa pombe ni rahisi sana kujitumbukiza katika masuala ya ulevi na uasherati hasa kutokana na kukosa kiigezo chema ndani ya familia yao hiyo. Watoto wenye wazazi ambao ni walevi huwa na matatizo ya kinafsi na kisaikolojia hasa maneno na istizai wanazofanyiwa na wenzi wao wakiwa skuli na maeneo mengine; hivyo watoto hao hujihisi kuwa na mapungufu na hata wakati mwingine mtoto huyo hufikia hatua ya kuogopa kujitambulisha kwamba, yeye ni mtoto wa fulani.
Hapana shaka kuwa, watoto ambao wazazi wao au mmoja kati ya wazazi wao wawili ni mlevi na mraibu wa pombe, huwa wameandaliwa uwanja wa kujitumbukiza katika vitendo vya ulevi. Hata hivyo wakati mwingine vitendo vibaya vya wazazi walevi huwa na taathira ambayo hubakia katika kumbukumbu za watoto hao na hivyo kuwafanya watoto hao kujiepusha na vitendo hivyo na hata yamkini watoto hao kutothubutu kutumia ulevi katika kipindi chao chote cha maisha yao kutokana na kushuhudia kitendo kibaya cha baba au mama yake alichokifanya hali ya kuwa amelewa na kitendo hicho kubakia katika kumbukumbu yake. Hata hivyo mifano ya watoto kama hawa ni michache mno. Ukweli wa mambo ni kuwa, ili kuhifadhi na kulinda misingi ya familia, kuna haja ya kuhifadhiwa thamani za kidini na kiutamaduni ambazo zimebinishwa katika jamii. Thamani hizo hupelekea kuweko mipango na utaratibu maalumu katika jamii na kuifanya jamii ifanye harakati katika njia sahihi na inayofaa. Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa utumiaji ulevi humfanya mhusika kutothamini au kuchunga thamani za kijamii na kidini. Kwani utumiaji pombe mbali na kukata uhusiano baina ya mja na Mwenyezi Mungu, huwa ni mwanzo wa kutumbukia katika uhalifu wa kijamii. Ni kwa kuzingatia uhakika huo ndio maana ikaelezwa kuwa, Mwenyezi Mungu ameharamisha ulevi, kutokana na kuwa pombe humuondolewa mlevi nuru katika moyo wake pamoja na insafu. Pombe humfanya mtu huyo kuwa na kiburi cha kufanya mambo ya haramu, umwagaji damu na kuchupa mipaka na akiwa amelewa, si jambo lililo mbali akamuingilia kimwili hata maharimu wake. Pombe haiongezi kitu zaidi ya mambo mabaya na machafu. Kwa muktadha huo inafahamika kuwa, pombe ni chimbuko la kila mambo mabaya na machafu na mlevi huweza kufanya jambo lolote bila kujali wala kufikiri natija na matokeo ya jambo hilo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …