Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 15 Januari 2012 12:15

Madhara ya Ulevi na Athari Zake (6)

Madhara ya Ulevi na Athari Zake (6)

Hii leo katika jamii tofauti utengenezaji, uzalishaji pamoja na matumizi ya pombe, yamekuwa yakienea kwa kasi licha ya kinywaji hicho kuharmisha na ushahidi wa tafiti mbalimbali unaoonyesha madhara ya matumizi ya pombe. Matumizi ya pombe katika mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu yameharamishwa na kupigwa marufuku na kuna riwaya na hadithi nyingi katika Uislamu ambazo zinasisitiza juu ya kuharamishwa kinywaji hiki. Hatua ya Uislamu ya kusisitiza juu ya kuharamishwa kunywa pombe inatokana na kuwa, pombe huwa na taathira hasi katika akili na fikra za mwanaadamu na kutokana na kinywaji hicho kulewesha hupelekea mwenye kuitumia kuwa na vitendo ambavyo si vya kawaida. Vile vile utumiaji pombe huwa na taathira mbaya katika utendaji tofauti wa mfumo wa mwili, ukiwemo mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, ini na mfumo mkuu wa neva. Fauka ya hayo, watoto wa watu ambao ni walevi huzaliwa wakiwa na matatizo sanjari na kurithi maradhi mabaya ikiwa ni pamoja na kuwa na nakisi katika baadhi ya viungo.
Ripoti na utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, utumiaji ulevi huwa na taathira mbaya mno kwa familia na jamii na wakati mwingine madhara yanayotokana na kutumia pombe huwa hayafidiki. Kutumia pombe ni moja ya sababu kuu zinazompelekea mhusika kutenda dhambi, jinai, kuua, kujiua na hata kifo wakati wa kuendesha gari. Hii inatokana na kuwa, pombe ni pango la kila madhambi. Wataalamu wa mambo wanasema kwamba, hii inatokana na kuwa, pombe huwa na taathira mbaya kiroho na kisaikoloji na humfanya mtumaiji kufanya mambo ya kihayawani ambayo yanakwenda kinyume kabisa na akili, utu na murua.
Pombe humfanya aliyeitumia kutokuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi sahihi na hivyo kumuandalia uwanja wa kutenda makosa na jinai.
Kila mwaka makumi kwa maelfu ya watu hurejea katika vyombo vya sheria kutoa mashtaka dhidi ya madereva waliowauwa watu wao wa karibu hali ya kuwa wanaendesha magari wakiwa wamelewa. Mtu aliyelewa hushindwa kuchukua maamuzi sahihi na kushindwa kubainisha baina ya baya na zuri. Aidha mtu aliyelewa hushindwa kufungamana na maadili mema pamoja na adabu na murua; na matokeo yake ni kufanya vitendo vya aibu na udhalili tena mbele ya kadamnasi. Kutoa matusi bila haya wala soni na kumtukana yeyote yule bila kujali rika wala uhusiano alionao ni moja ya athari ya wazi mbaya ambayo huonekana kwa mlevi. Mlevi humtusi na hata kumvunjia heshima baba na mama yake mzazi bila kujali. Bwana Mtume Muhammad SAW anasema kuwa, "pombe ni chimbuko la madhambi na ni chemchemi na ufunguo wa kila mambo mabaya na machafu". Kwa muktadha huo, pombe ni sababu na chimbuko la kila shari, madhambi na mambo yote machafu na ya udhalili.
Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa, nchini Marekani matumizi ya pombe yamekuwa na nafasi ya asilimia 30 katika ubakaji na asilimia 75 katika utumiaji mabavu na kuwapiga wanawake. Katika nchi za Magharibi hususan nchini Marekani sio tu kwamba, hakuchukuliwi hatua zozote za kukabiliana na matumizi ya pombe na ulevi, bali katika mashindano mengi ya michezo na vipindi cha Televisheni kumekuweko na matangazo ya kuvutia na yaliyogharimu fedha nyingi kwa ajili ya kutangaza matumizi ya kinywaji hiki chenye kudhuru.
Nchini Russia matumizi ya pombe yameongezeka kwa kasi, kiasi kwamba, baadhi ya wataalamu wa mambo nchini humo wanasema kuwa, tatizo la ulevi nchini humo limegeuka na kuwa maradhi. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa wastani kila raia wa Russia kwa mwaka hutumia lita 18 za pombe. Aidha katika miezi sita ya awali ya mwaka 2009 ajali elfu tano zilizopelekea mauaji ya watu elfu nane nchini Russia chanzo chake kilitokana na madereva kuendesha magari wakiwa wamelewa. Ili kukabiliana na ongezeko la matumizi ya pombe viongozi wa Russia waliamua kupandisha bei ya pombe wakidhani kwamba, kwa kufanya hivyo matumizi ya pombe katika nchi hiyo yatapungua.
Moja ya asasi zinazoathirika zaidi na utumiaji ulevi ni familia. Takwimu zinaonyesha kuwa, utumiaji ulevi katika familia hupelekea kusambaratika misingi na nguzo za familia. Hii ni kutokana na kuwa, baba au mama mlevi hutumbukia katika ulevi na kuwatelekeza watoto. Aidha katika jamii nyingi tunashuhudia ndoa kuvunjika, familia kusambaratika na hata watoto kutekelezwa kutokana na wazazi au baba ambaye ndiye msimamizi mkuu wa familia kuwa mraibu wa pombe na hivyo kutoitunza familia. Ni kwa kuzingatia ukweli huo ndio maana, walevi wanahesabiwa kuwa mfano mbaya kabisa katika familia. Vile vile utumiaji wa ulevi, huhatarisha usalama wa uchumi wa familia. Kwa kuzingatia kwamba, familia hukidhi mahitaji yake kupitia kwa baba au mama kufanya kazi au msimamizi mhusika wa familia, hivyo inapotokea wahusika hao kuwa walevi, huacha majukumu yao ya kukidhi mahitaji na hawaiji za familia zao na huo kuwa mwanzo wa kusambaratika familia kutokana na wanafamilia kuondokewa na chanzo chao cha kipato.
muundo wa familia. Hadi tutakapokutana tena wiki ijayo, ninakuageni nikikutakieni kila la kheri. Kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …