Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 15 Januari 2012 12:13

Ulevi, Madhara na Athari Zake (3)

Miongoni mwa sifa maalumu na za kipekee za mafundisho aali ya dini tukufu ya Kiislamu ni mafundisho hayo kwenda sambamba na dhati ya utakasifu wa kibinaadamu. Sheria na mafundisho ya dini ya Kiislamu, ni majimui jumla ya mafundisgo ambayo, Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume wake ili waje kumuongoza mwanaadamu kuelekea katika saada na ufanisi. Mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu yamezingatia pande zote za mahitaji ya mwanaadamu katika maisha yake na hata sheria ambazo zinamkataza mwanadamu kufanya baadhi ya mambo nazo pia zimezingatia maslahi ya kiumbe huyu yaani mafundisho hayo yanazingatia madhara na faida ya kitu hicho kwa mwanaadamu. Kwa muktadha huo, hakuna kitu katika mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu ambacho kimehalalishwa au kuramishwa bila ya kuweko hoja na hekima ndani yake. Mwanaadamu mwenye kumpewekesha Mwenyezi Mungu anaamini kwamba, sheria hizi zimetoka katika elimu ya Mwenyezi Mungu isiyo na kikomo, Mwenyezi Mungu ambaye ana ujuzi wa kila kitu. Imam Ali bin Mussa Ridha AS mmoja wa Maimamu wa watu wa Nyumba Tukufu ya Bwana Mtume SAW anasema kuwa, hakuna chakula au kinywaji ambacho Mwenyezi Mungu amekihalalisha isipokuwa amezingatia suala la maslahi na manufaa yake; na hakuna kitu ambacho amekiharamisha isipokuwa amezingatia suala la madhara na maangamizo yake. " Mafundisho ya Kiislamu yamezingatia engo na pande zoite za maslahi ya mwanaadamu iwe ni upande wa kimwili na kiroho au upande wa mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Mipango mingi ya dini sio tu kwamba, inasafisha na kuitakasa roho ya mwanaadamu, bali inaukinga mwili na madhara na ufisadi. Mfano wa hilo ni kama suala la kuharamishwa ulevi.
Matumizi ya ulevi katika dini tukufu ya Kiislamu yameharamishwa kutokana na kuwa, kitendo cha kutumia ulevi kinatishia na kuhatarisha uzima wa mwili na roho na hata usalama wa jamii. Wasomi na wataalamu wa elimu ya tiba na wa masuala ya kisaikolojia wamesema mengi kuhusiana na madhara na athari za utumiaji ulevi katika nyanja mbalimbali za maisha.
Baadhi ya asasi za kijamii pia zimefanya utafiti mwingi kuhusiana na madhara ya ulevi na athari zake. Hivi karibuni Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Uraibu cha Marekani kilitoa takwimu zinazohusiana na utumiaji ulevi unaofanywa na wanafunzi wa Kimarekani. Kituo hicho kilitangaza kuwa, wanafunzi milioni 13 wa Kimarekani kwa akali wamewahi kutumia madawa ya kulevya au pombe mara moja. Kwa mujibu wa takwimu hiz0 ni kuwa, katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2005 utumiaji ulevi baina ya vijana chipukizi wa Kimarekani uliongezeka mno. Kituo hiki kimezitaka familia, maafisa wa elimu na hata wanasiasa wa Marekani kuonyesha radiamali yao kuhusiana na mwenendo huu hatari na unaokithiri wa utumiaji madawa ya kulevya na pombe katika skuli za Marekani. Utafiti uliofanywa na wataalamu unaonyesha kwamba, utumiaji ulevi unasababishwa na sababu mbalimbali ambapo mojawapo tunaweza kuashiria masuala ya hali ya wasi wasi, fadhaa, msononeko na kutojiamini au jitihada za kukimbia hali ya fadhaa na kuchanganyikiwa kiakili kwa kiwango fulani. Baadhi ya watu wakati wanapokuwa na hali ya wasi wasi wakiwa na lengo la kutafuta hali ya utulivu huamua kunywa pombe au kutumia ulevi wakijidanganya kwamba, wakiwa wamelewa wanaweza kukweka hali ya mawazo, msononeko na kujiinamia wanayokabiliwa nayo. Ukweli wa mambo ni kuwa, katika hatua ya awali, mlevi hupata hisia ya uongo, lakini baada ya muda, athari mbaya za kutumia pombe huanza kudhihirika.
Miongoni mwa athari za wazi kabisa za mtu aliyetumia kileo ni kuyumba, kushindwa kuchukua maamuzi na kuzungumza maneno yasiyo na maana. Utafiti uliofanywa unaonyesha kwamba, wanawake huathirika zaidi na athari mbaya za pombe ikilinganishwa na wanaume. Maafa yaliyoathiri jamii za kibinadamu kwa kutokana na utumiaji wa ulevi ni makubwa kuliko hata majeraha yanayotokana na magonjwa hatari. Wanasayansi waliobobea wanaamini kuwa, utumiaji wa ulevi huleta magonjwa mabaya kabisa ya kansa ya tumbo na maini, magonjwa ya tumbo, kifua kikuu, magonjwa ya akili kama vile ukichaa na kadhalika na kuharibu vizazi kwa kuathiri viungo kuanzia tumboni na mamilioni ya maovu yanayotokana na ulevi. Kwa hakika pombe ni sawa na sumu na hivyo hakuna mtu yeyote atakayesema kuwa sumu kwa kiwango kidogo hakidhuru .Leo hii wanazuoni wengi wanatilia mkazo juu ya suala hili na kusisitiza kuepukana na matumizi ya ulevi ambayo yamepelekea familia nyingi kusambaratika. Hatari nyingine inayowakumba walevi ni kule akili na seli za fahamu zao huharibiwa vibaya kabisa na huweza kupatwa na magonjwa ya kila aina. Profesa mmoja kutoka Chuo kikuu cha Tehran anasema kwamba: "Ulevi ni aina mojawapo na mihadarati ambayo inayodhuru mishipa ya fahamu. Inadhuru seli za bongo na kusababisha ukichaa na hata mtu kuwehuka" Imam Ridha AS anasema kuwa, Mwenyezi Mungu ameharamisha ulevi wa kila aina kwa sababu ya maovu yasababishwayo nayo na kwa sababu huharibu ufahamu na busara za mwanadamu na huondoa wema na heshima."

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …