Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 15 Januari 2012 12:12

Ulevi, Madhara na Athari Zake (2)

Pombe na baadhi ya vileo mfano wake kutokana na kuwa na mada inayojulikana kwa jina la alkoholi huwa na sifa ya kulewesha na kudhoofisha. Mada ya kemikali ya alkoholi ilikuwa ikijulikana na mwanaadamu tangu kale. Karne kadhaa zilizopita, msomi wa Kiislamu aliyejulikana kwa jina la Muhammad bin Zakaria Razi aliyefariki dunia katika karne ya nne Hijria alifanikiwa kugundua mada ya kemikali ya alkoholi ambayo huweza kutumika katika masuala mbalimbali ya kitiba. Katika zama zetu hizi mada ya kemikali ya alkoholi ina matumizi mengi hasa katika uga wa tiba, katika masuala ya kuchangaya dawa.
Alkoholi hutumika pia kuzuia kukua kwa vijidudu. Vile vile leo hii alkohili inatumika kwa ajili ya kutibu vidonda na kuzuia vijidudu kuingia katika vidonda. Ulevi ni kinywaji ambacho ndani yake kina mada ya alkoholi. Hii ina maana kwamba, kabla ya kinywaji hicho kutiwa mada ya alhkoli ni halali kunywa kama ambavyo leo kuna vinywaji vingi vya mchanganyiko wa matunda ambavyo vimetengenezwa kutokana na ngano ambavyo huwa havina mada ya alkoholi; hivyo si haramu kunywa kinywaji kama hiki ambacho kimsingi hakileweshi.
Hii leo inasikitisha kuona kuwa, utumiaji ulevi na matumizi ya baadhi ya vinywaji ambavyo vina alkohili ndani yake, limegeuka na kuwa jambo la kawaida katika jamii nyingi za ulimwengu wa Magharibi.
Kinyume na wanavyodhani baadhi ya watu, utumiaji ulevi hauimarishi viungo vya mwili, bali taathira yake ya kulewesha hudhoofisha mwili pamoja na kupunguza umakini katika kufanya kazi mbalimbali hasa zinazohitajia akili na kufikiri.
Wataalamu katika uwanja huu wanasema kwamba, hii kwamba, mlevi hukosa haya na hata huweza kusema na kufanya mambo ambayo akiwa hajalewa hawezi kuyafanya haitokani na kuwa utumiaji pombe humpa mtu nguvu n ujasiri, la hasha bali vitendo anavyovifanya vinatokana na taathira ya kudhoofishwa vituo vya ubongo na akili baada ya kutumia ulevi. Maneno na vitendo anavyovifanya ni taathira mbaya ya ulevi. Hivyo basi, vileo vyote vina mada ya kemikali na athari yoyote ya kulevya inayotokana na kinywaji hicho inatokana na kuweko kwa kwa alkoholi.
Taathira muhimu ya alkoholi katika mwili wa mwanaadamu, ni kudhoofisha sehemu za neva yaani mshipa wa ufahamu katika mwili wa mwanaadamu na ubongo. Taathira hiyo katika mishipa ya ufahamu hupenya na kufika katika mishipa ya damu kiasi kwamba, huvuruga mzunguko wa kawaida wa damu na wakati mwingine athari hizo hufika hadi katika ngozi ambapo baadhi ya wakati ngozi ya mlevi huwa nyekundu.
Wataalamu wa mambo wanasema kuwa, awali kileo huleta joto kwa mtumiaji ambapo baada ya muda mchache joto hili hupanda na huongezeka na kuna vitendo vyake huongezeka, mapigo ya moyo huenda kwa kasi na hupumua haraka haraka. Baada ya hatua hiyo athari zake kileo hicho hupenya na kufika katika mishipa ya ubongo au mishipa ya ufahamu na hivyo utamuona anaanza kuzungumza sana kupita kiasi huku akikariri sentesi moja na kusisitioza mara kadhaa na wakati mwingine kusahau kwamba alikwisha sema neno hilo punde tu. Athari nyingine ni katika mishipa ya nguvuza kusikilizia. Inaelezwa kuwa kileo kikifika mahala hapo, mtu aliyetumia kileo huanza kusikia sauti asizozielewa na hta wakati mwingine kuitika akidhani kwamba, kuna mtu amemwita. Hatua inayofuata ni vituo vya kutazamia na hivyo utamuona mtu aliyelewa akitazama kitu mara mbili mbili na wakati mwingine kushindwa kufahamu hasa kitu hicho ni nini. Dr. Melvin Kanzeli, ambaye amepitisha miaka mingi katika utafiti juu ya unywaji wa pombe, anasema kuwa, "Unywaji wa pombe unaharibu sana ubongo wa mtu. Wakati mtu anapojiona kuwa anasikia raha na kuburudika kwa kiwango kidogo cha pombe, huwa hana habari kuwa anaziua seli za ubongo wake." Dr. Kanzeli ambaye ndiye Mkuu wa taasisi ya utafiti cha Chuo cha Matibabu cha South Carrolina, anaamini kuwa ulevi huasababisha mabadiliko katika damu na mishipa yake kiasi kwamba, ubongo unakosa hewa ya oksijeni na hivyo kuharibiwa, au huharibika kiasi kwamba, mtu anatumbukia katika hali ya kuchanganyikiwa akili.
Kuingia kwa pombe katika damu kunaathiri mno mzunguko wa damu, na hivyo mara nyingi husababisha kuganda kwa damu. Dr. Hertbert Moskov, tabibu mashuhuri wa nchini Russia anasema kwamba, "Pombe hudhoofisha seli za ubongo na kuteketeza nguvu za uwezo wa kukabiliana na matatizo. Lakini tatizo kubwa ni dosari za urithi wa kimwili. Mlevi kwa kawaida huwa amechoka, mvivu na mpumbavu. Yeye huwa hayupo tayari kusoma na daima huwa amelaaniwa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …