Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 15 Mei 2012 12:52

Somo la Khamsini na Mbili

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi hiki cha kujifunza lugha ya Kifarsi. Ni furaha yetu kuwa umejiunga nasi katika somo letu la leo ambalo ni la 52 katika mfululizo wetu huu. Leo tutazungumzia utamaduni wa Wairani wa kuwaheshimu watu wa makamo na wenye umri mkubwa. Wairani huwaheshimu sana watu wazi na walio na umri mkubwa na hasa babu na nyanya yaani bibi na daima huwatembelea ili kuwajulia hali zao. Katika aghalabu ya famili, wazee hao huishi pamoja na wajukuu zao. Mazungumzo ya kipindi chetu cha leo yatahusu ada hii ya kupendeza ya Wairani. Mohamad na rafiki yake Hamid wako kwenye maktaba. Hebu sasa tusikilize mazungmzo yao lakini kwanza tujifunze misamiati muhimu itakayotumika leo.
Sikiliza kwa makini
Kesho----Ijumaa---mpango gani--- wewe una mpango gani---nyumba----babu---nyanya au bibi---mjomba دایی---- mama mdogo----mama-- baba----dada mimi ninaenda---wao wanaishi----Qazvin----Tehran---mbali---gari----masaa mawili---kila wiki----wewe unaenda---kuona---hapo----yeye amesema---yeye ni mgonjwa---ugonjwa---kidogo---wao wanakuja---Wairani---Sisi tunaenda----wakubwa (kwa umri)-(au watu wa makamo)-simu---piga simu----kwa kawaida---yeye atapiga simu---kila siku---haitoshi----daima---yeye huenda----yeye anaishi---kuona---utamaduni---heshima---agiza au himiza---kuwaheshimu
***
Sasa sikiliza mazungmzo yao kwa makini.
Effect (صدای ورق زدن كتاب ))
Mohammad: Hamid, una mpango gani kwa ajili ya kesho ijumaa?.
Hamid: Nitaenda nyumbani kwa babu.
Mohammad: Nyumba ya babu yako iko Tehran?
Hamid: Hapana. Wao wanaishi Qazvin.
Mohammad: Qazvin iko karibu na Tehran?
Hamid: Si mbali sana. Masafa ya masaa mawili kwa gari.
Mohammad: Kila wiki wewe huenda katika nyumba ya babu yako?
Hamid: Ndio. Ndio, mimi huenda huko kwa ajili ya kuwaona babu na nyanya yangu. Mama amesema, nyanya ni mgonjwa kidogo.
Mohammad: Utaenda huko peke yako?
Hamid: Hapana. Baba, mama na dada yangu pia watakuja. Sisi Wairani daima huenda kuwatembelea watu wazima.
Mohmmad: Ni kazi nzuri. Lakini Qazvini ni mbali. Piga simu!
Hamid: Simu!? Mama yangu humpigia nyanya simu kila siku. Lakini simu haitoshi.
Mohammad: Mjomba pia daima huenda kuwatembelea babu na nyanya?
Hamid: Ndio. Katika utamaduni wetu kuwaheshimu wakubwa kwa umri ni jambo linalohimizwa.
Mohammad: Ni vizuri sana kuwa kuwatembelea wazee na kuwaheshimu ni jambo la kawaida nchini Iran.
***
Sasa sikiliza mazungumzo hayo lakini bila tafsiri ya kiswahili.
....****
Kama ambavyo umesikia katika mazungumzo hayo ya Mohammad na Hamid, Wairani huwaheshimu sana wazee na watu wa makamo na daima huenda kuwatembelea. Katika sherehe mbali mbali kama siku za Iddi, wadogo katika familia huwatembelea wazee. Kisha baada ya hapo wazee nao huwatembelea watoto na hivyo kuimarisha nguzo za familia katika jamii. Hakuna shaka kuwa katika nchi yako pia kuna mila na desturi zinazopendeza za kuwaheshimu wazee. Sisi hapa pia tunawausia kuwaheshimu wazee wenu kwani wana uzoefu mkubwa na wanawapenda.
Tunakomea hapa kwa leo. Tungependa kuwakumbusha kuwa anuani yetu ya intaneti ni kiswahili.irib.ir
Hadi tutakapokutana tena kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …