Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 17 Aprili 2012 11:37

Somo la Khamsini na Saba

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizahi na karibuni katika kipindi hiki mkipendacho cha kujifunza luga ya Kifarsi. Jiunge nasi leo katika somo hili letu la 57 ili tuweze kuenda katika sehemu moja maridadi na ya kuvutia Tehran. Medani ya Tajrish ni moja ya medani kongwe zaidi kaskazini mwa Tehran na kuna soko la kale hapo. Kusini mwa medani hiyo kuna Haram Takatifu ya Imam Zadeh Saleh. Imam Zadeh Saleh ni kaka yake Imam Reza (AS). Haram hii iko katika jengo la kale na maridadi na embizoni mwake kuna bustani la kuvutia pamoja na bwawa liloja maji. Wakaazi wa Tehran na hata watu kutoka miji mingine huja kwa ajili ya Ziara na kuswali katika sehemu hii takatifu. Mohammad na rafiki yake, Hamid leo wako katika medani ya Tajrish. Ni wakati wa adhuhuri na Mohammad anasikia sauti ya Adhana. Kutokana na kusikia sauti hiyo anafahamu kuwa Msikiti uko karibu na walipo. Kwa hivyo kwa pamoja anaenda na Hamid katika Haram ya Imam Zadeh Saleh. Basi tuandamane nao katika sehemu hiyo takatifu. Lakini kwanza tujifunze misamiati muhimu itakayotumiak katika kipindi cha leo.
****
Sauti---Adhana----Msikiti---Haram---Imam Zadeh Saleh (Kaka yake Imam Reza-as)---Teunde---Tusome بخوانيم ( hutumika pia kumaanisha kuswali)---Pale---hapa---tizama----sisi tunaweza kuswali---Nani?----Kaka----Imam Reza----Wajukuu----Mtume wa Uislamu-----Medani---Medani ya Tajrish---Msongamano--- Maridadi---Maridadi sana----watu----wao wanakuja---- ziara----sala---- Jengo----kale---Vizuri sana!---Maktaba---- ubao----kutumia--- wote
(zinagatia: Mimi ninasoma---- mimi ninaweza kusoma---sisi tunasoma----sisi tunaweza kusoma-----wao wanasoma-----wao wanaweza kusoma)
Mwendeshaji: Sasa sikiliza mazungmo ya Mohammad na Hamid. Jaribu kurudia tena sentensi za Kifaris.
***
Mohammad: Sauti ya Adhana inasikika. Msikiti uko wapi? Tuende tuswali.
Hamid: Tizama pale. Pale ni Haram ya Imam Zadeh Saleh. Tunaweza kuswali katika Haram.
Mohammad: Imam Zadeh Saleh ni Kaka ya Imam Reza. Imam Reza ni kati ya wajukuu wa Mtume wa Uislamu.
Hamid: Harama ya Kaka ya Imam Reza Iko hapa?
Mohammad: Ndio. Haram ya Imam Zadeh Saleh iko katika medani ya Tajrish.
Mwendeshaji: Sasa sikiliza mazungmzo hayo ya Mohammad na Hamid alikini bila tafsiri ya Kiswahili....
****
Mohammad na Hamid wanaelekea katika Haram na kuingia katika eneo lake la nje. Mohammad anastaajabu na kuangalia hapa na pale. Kuna msongamano mkubwa kwnai watu wengi wamekuja kufanya ziara. Anawaona watu wakitia udhuu ili waswali. Mohammad anavutiwa pia na kuona maktaba iliyo hapo...

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …