Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 17 Aprili 2012 10:58

Somo la Tisini na Tano

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 95. Iwapo unakumbuka katika kipindi chetu kilichopita, Mohammad alienda kumona daktari Bi. Ramadhani kutokana na maumivu ya kichwa na hisia ya ugonjwa mwilini. Daktari alimtaka Mohammad achukue kipimo cha damu. Baada ya kuchukia natija ya kipimo, Mohammad leo anaenda kumona daktari. Anapofika kliniki anaona hakuna wagonjwa wengi na punde si punde anaingia katika chumba cha daktari. Jiunge nasi tusikilize mazungmo ya Mohammad na Daktari Bi Ramazani. Lakini kwanza tujifunze misamiati muhimu itakayokutmika katika somo la leo. Tafadhali zingatia.
$$4
Karibu----خوش آمدید - بفرمایید Karibu---juzi---kwa ajili---maumivu ya kichwa----nilikuja kukuona----sasa-jawabu----kipimo cha damu----mimi nimeleta---nina kumbuka----bora zaidi----imekuwa---Mimi nime borekaمن بهتر شدم ---- lakini----tembe----sherbati----bado----mimi ninakula----tafadhali---jawabu-----kipimo----leta----nione----nashukuru----mushkili---maalumu----kawaida----mafuta katika damu----Namshukuru Mola---mimi sina----kidogo-----hofu----mimi nilikuwa----kwa nini----wewe umekuwa----wewe ni---kijana---chipukizi سرحال -----kula---dawa---madawa----mimi nitaendelea---mimi niendelee---kula---keshokutwa----iwapo----wewe haukuwa na----kata.
$$
Sasa sikiliza mazungmzo ya Mohammad na Dkt. Bi Ramazani.
Dkt. Hujambo. Karibu. Vipi hali yako?
Mohammad: Bi. Daktari. Juzi nilikuja kukuona kwa ajili ya maumivu ya kichwa na sasa nimeleta jibu la kipimo cha damu.
Daktari: Ndio. Ninakumbuka. Maumivu ya kichwa chake yameboreka?
Mohammad: Ndio. Nimeboreka. Lakini ningalu ninatumia tembe na sharbati.
Daktari. Tafadhali leta jawabu la kipimo chako nione.
Mohammad: Hii hapa bi daktari.
Bi. Daktari: Nashukuru (sauti ya makaratasi). Hauna mushkili maalumu. Mafuta yako ni ya kawaida.
Mohammad: Nina mshukuru Mola kuwa sina mafuta mengi katika damu. Nilikuwa na wasi wasi kidogo.
Daktari: Kwa nini ulikuwa na wasi wasi? Wewe ni kijana na ni chipukizi.
Mohammad: Bi Daktari niendelee kutumia dawa?
Daktari: Ndio. Endelea kutumia dawa hadi keshokutwa. Iwapo hautakuwa na maumivi ya kichwa, katika matumizi ya dawa.
Mohammad: Nashukuru Bi Daktari.
$$
Kwa mara nyingine sikiliza mazungmzo ya Mohammad na Bi Daktari lakini bila tafsiri ya Kiswahili.
$$
Daktari hamuandikii Mohammad dawa. Mohammad anaaga na kuondoka katika kliniki. Anafurahi kuwa baada ya kipimo cha damu amepata yakini kuwa afya yake ni nzuri. Dawa alizagizwa kutumia na daktari zimemsaidia. Mohammad sasa anaweza kutulia katika masomo yake na kujitayarisha kwa ajili ya mtihani. Akiwa njiani kuekeleka katika bweni ananunua mkata na matunda. Sisi pia tuna furaha kuwa Mohammad hana tatizo nyeti la kiafya. Hapa studioni Tunakutakieni nyote afya na salama. Kipinsi hiki kinapatikana katika ukurasa wetu wa intaneti ambao ni This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. .
Kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …