Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 17 Aprili 2012 10:52

Somo la Tisini na Sita

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibu kujiunga nasi katika kipindi  hiki cha kujifunza lugha ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 96. Mohammad na Saeed wamekubaliana kuwa siku ya Ijumaa wataenda katika mgahawa ili kula chakula kitwacho Fesenjan ambacho ni kati ya vyakula vya kipkee vya Kiirani. Fesanjan ni mchuzi mtamu ambao huliwa pamoja na wali. Mchuzi huo hujumuisha nyama ya kima, jozi zilizosagwa, kitunguu na komamanga. Chakula hiki kitamu cha Kiirani hutumika sana katika karamu na sherehe za harusi. Fesanjan hutayarishwa kwa njia tafatui katika miji mbali mbali ya Iran. Kabla ya kusikiliza mazungmzo ya marafiki hao wawili hebu kwanza tujifunze misamiati muhimu ya kipindi cha leo.
Tafadhali zingatia.
Unakumbuka-----Ijumaa----Mgahawa----Wewe ulisema-----sisi tunaenda----hivi sasa----nakumbuka----mimi nilikuwa nimesahau----kesho----chakula cha mchana-----ni vizuri------ipi----Mgahawa wa Raftari----tamu لذیذ ---chakula----maalumu----mchuzi خورش -----fesanjan----ni nini?----hadi sasa----mimi sijala------nyama----jozi----sosi ya komamanga-----wao hupika----wali-----wao hula----chacha----yeye ana----hivyo----kiasi---- sukari----wao hutia----tamu ----شیرین huko nyuma----Kiirani----mimi nilikuwa---mimi ninauhakika-----unapendezwa----mim nitajaribu----wao wanapenda----zaidi----ugeni----juu ya----meza---meza ya maakuli-
@@@
Sasa sikiliza kwa makini mazungmzo ya Mohammad na Saeed ambao wako barabarani wakitembea.
Effect: صدای تردد ماشینها در خیابان
Mohammad: Unakumbuka ulisema Ijumaa tutaenda mgahawani?
Saeed: Ndio. Nimekumbuka sasa hivi. Nilikuwa nimesahau. Kesho tutaenda mgahawani kwa ajili ya chakula cha mchana.
Mohammad: Ni vizuri. Tutaenda mgahawa upi?
Saeed: Katika Mgahawa wa Raftari. Chakula cha mgahawa huu ni kitamu sana, hasa mchuzi wa Fesanjan.
Mohammad: Mchuzi wa Fesanjan ni nini? Hadi sasa sijaula mchuzi huu.
Saeed: Mchuzi wa Fesanjan unapikwa kwa Jozi, nyama na sosi ya komamanga na huliwa kwa wali.
Mohammad: Fesanjan ina sosi ya komamanga? Kwa hivyo ni chachu.
Saeed: Hapana. Si chachu sana kwa sababu hutiwa sukari kiasi, ina noga.
Mohammad: Huko nyuma nimewahi kula michuzi ya Kiirani. Kawaida huwa chachu kidogo.
Saeed: Ndio. Lakini Fesanjan ni tamu. Nina uhakika utafurahia.
Mohammad: Wairani wanapenda Fesenjan, katika karamu nyingi Fesenjan huwa katika meza ya maakuli.
@@@
Kwa mara nyingine tena sikiliza mazungmzo hayo kwa lugha ya Kiswahili.
@@@
Basi siku ya Ijumaa Mohammad na Saeed wanaenda katika mgahawa ambao hupika chakula cha kienyeji katika moja ya maeneo ya kale ya Tehran. Wanafika mgahawani hapo na kupata wateja wengine wengi, wanaagiza Fesanjan , mtindi na saladi. Wakali chakula kinapoletwa mezani Mohammad anavutiwa na rangi ya kahawia ya Fesanjan. Hakudhani itakuwa na rangi hiyo. Anafurahia sana chakula hicho na kusema ndio chakula kitamu zaidi cha Kiirani alichowahi kula. Ni matumaini yangu kuwa wewe pia utapata fursa ya kuja hapa Iran na kula vyakula mbali mbali na vitamu vya Kiirani.
Tunafikia tamati hapa kwa leo, unaweza kusikiliza kipindi hiki kupitia tovuti yetu ambayo ni Kiswahili.irib.ir

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …