Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 12 Aprili 2012 17:28

Somo la Mia Moja na Sabiini na Nne

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nasi tena katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Hili ni soma la 174. Leo tunaarifisha Bustani ya Kitaifa ya Golestan. Katika somo lililopita Mohammad na Romin ambao wako safarikini mkoani Golestan waliamua kuandamana na rafiki yao Sadeq katika kutembelea Bustani ya Kitaifa ya Golestan. Bustani hiyo iko katika lililohifadhiwa mashariki mwa mkoa wa Golestan na magharibi mwa mkoa wa Khorassan. Bostani hii ni moja kati ya bustani za kale na kubwa zaidi Iran. Bustani ya Golestan yenye ukubwa wa kilomita mraba laki tisa na ina wanyama na mimea mbali mbali nadra. Kati kati ya bustani hiyo kuna barabara inayopita kuelekea mji mtakatifu wa Mashhad. Wafanyaziara wengi katika haram ya Imam Redha AS hupita njia hii kutokana na umaridadi wake. Mohammad, Romin na Sadeq wako katika Bustani hiyo hivi sasa. Kabla ya kusikiliza mazungumzo yao hebu tujifunze misamiati muhimu itakayotumika katika somo la leo.
@@@
Barabra----maridadi----kijani kibichi----nyingi-----bustani----takribani-----kijiji-----Tangrah-----Hiyo inaanzia-----kale zaidi-----Bustani ya Kitaifa-----Inaelekea kuwa----hapa----kimaumbile asilia-----kale-----bila shaka ----mnyama----wanyama-----mbali mbali----wao wanaishi-----anua----spishi (wa wingi)----mmea---ya mimea----kuna----sana----kubwa-----ni vivyo hivyo-----900 kilomita mraba-----ukubwa-----ya kuvutia-----kati kati-----hiyo hupita-----mazingira------eneo-----athari----hasi---hiyo huacha----ni sahihi---mto----maporomoko ya maji----Agh Soo----Maporomoko ya Msitu wa Golestan----Muinuko----Mita 80----Maarufu----sasa au inayotiririka----leo usiku----sisi tubaki----hatari----mwitu----hiyo hutishia---mahala-----taa----hiyo inawaka----sisi tunaweza kupumzika----ni vizuri------mimi ninapenda kuchuma---pea za msituni----
@@@
Sasa tusikilize mazungumzo ya Mohammad na Sadeq kuhusu Bustani ya Kitaifa ya Golestan
@@@
Mohammad: Ni barabara maridadi! Misituhuu ni kijani kibichi na umejaa.
Sadeq: Bustani hii takribani inaanza baada ya kijiji cha Tangrah. Hii ni bustani ya kale zaidi Iran.
Mohammad: Inaelekea kuwa hapa ni msitu wa maumbile asilia na wa kale. Basi bila shika kuna wanyama wengi waishio ndani yake.
Sadeq: Ndio. Katika bustani hii kuna anua ya wanyama na spishi za mimea.
Mohammad: Basi bustani hii ni lazima iwe kubwa sana.
Sadeq: Ndio. Ni vivyo hivyo. Bustani hii ina upana wa kilomita mraba 900.
Mohammad: Bila shaka msitu huu mkubwa ni maridadi na wa kuvutia.
Sadeq: Lakini kuna barabara inayopita katikati ya msiku na kuacha athari mbaya katika mazingira ya eneo.
Mohammad: Ni sahihi. Je kuna mto na maporomoko ya maji katika bustani hii.
Sadeq: Ndio kuna maporomoko ya maji ya Agh Soo na maporomoko ya maji ya Msitu wa Golestan yenye muinuko wa mita 80 na ni kati ya maporomoko maarufu ya ustani hii. Aidha kuna mito inayotiririka katika bustani hii.
Mohammad: Iwapo leo usiku tutabaki katika bustani kuna hatari ya wanyamwa wa mwitu?
Sadeq: Hapana. Tunaweza kupumzika katika mahala ambapo taa zimewaka.
Mohammad: Vizuri. Mimi napemda kuchuma pea za msitu.
@@@
Sasa sikiliza mazungmzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.
@@@
Mpenzi msikilizaji ni matumaini yetu kuwa ukipata fursa ya kutembele Iran bila shaka utafika katika bustani maridadi ya Golestan. Kipindi chetu kinafikia tamati hapa kwa leo. Unaweza kututumia maoni yako kupitia email yetu ambayo ni This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. . Kipindi hiki kinapatika katika tovuti yetu ya http://iswahili.irib.ir
Kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …