Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 12 Aprili 2012 17:26

Somo la Mia Moja na Sabiini na Tatu

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo hili ni la 173. Leo tutasafiri hadi mkoa wa Golestan. Kimsingi, kwa lugha ya Kifarsi, Golestan ni jina la eneo lenye maua na mimea mingi. Kwa hivyo jina la mkoa huu linaashiria eneo la kijani kibichi na maridadi. Mohammad na Romin wameamua kwa pamoja kuenda katika mji wa Gorgan ambao ndio makao makuu ya mkoa wa Golestan. Wanataka kumtembelea rafiki wao wa pamoja ambaye jina lake ni Sadiq aliyewaalika katika wakati wa likizo. Babu yake Sadeq anaishi katika kijiji kimoja maridadi cha Golestan kiitwacho Ziyarat. Asubuhi na mapema wanachukua basi kuelekea Gorgan na masafa ya mji huo na Tehran ni takribani masaa matatu na nusu. Wakiwa njiani kuelekea eneo hilo la kaskazini mwa Iran wanapita maeneo ya kijani kibichi hadi wanapofika katika mkoa wa Golestan ulio katika pwani ya Bahari Kaspi. Mji wa Gorgan ni mkubwa na wa kihistoria ambao umekuwepo kwa takribani miaka elfu mbili. Kabla ya kuendelea tujifunze misamiati muhimu ya leo.
@@@
Hatimaye-----mji-----Gorgan-----Sisi tumefika----choka---kwa sadfa----mandhari----maridadi----pembeni----barabara----mimi nimefurahia----kiasi gani----mkoa-----Mazandaran-----Golestan----Kijani Kibichi-----Sana----Hizo zinatafutiana----unaweza kusema-----eneo---sehemu----kinyume----hewa-hapa-----nyevu----kutokana na kuwa----Bahari ya Kaspi----Karibu----Kidhahiri----Kubwa----Leo----Sisi tutabaki-----hatubaki-----baada ya adhuhuri-----Bustani ya Golestan-----Sisi Tutaenda----Wapi?----Njia----Barabara----Mashhad----Hiyo iko-----mimi nina uhakika-----tafrija----siku ya kualiwa kwako utabeba----mpenzi----maumbile asili----hasa----kama hii----mandhari----baadhi----msafiri---wao wanapita----usiku------wao wanakaa----sisi wenyewe----hema----kidogo----vifaa vya dharura----sisi tubebe-----sisi tubaki
@@@@
Sasa tusikilize mazungmzo ya Mohammad na Romin ambao punde hivi wameshuka kutoka basi. Tafadahili Zingatia.
Romin: Hatimaye tumefika katika mji wa Gorgan. Hujachoka?
Mohammad: La. Kwa sadfa zimefurahia mandahri maridadi njiani. Mikoa ya Mazandaran na Golestan ni kijani kibichi sana.
Romin: Ndio. Mikoa hii inatafautiana sana na Tehran. Unaweza kusema eneo hili ndio sehemu ya kijani kibichi zaidi Iran.
Mohammad: Kinyume na Tehran ambapo hali ya hewa ni kavu, hapa hali ya hewa nyevu.
Romin : Ndio. Ni kwa sababu mikoa hii iko karibu na Bahari ya Kaspi.
Mohammad: Kidhahiri Gorgan ni mji mkubwa. Leo tutabaki hapa>
Romin: La. Hatutabaki mjini. Baada ya adhuhuri tukiwa na Sadeq tutaenda Bustani ya Golestan.
Mohammad: Bustani ya Golestan Iko Wapi?
Romin: Bustani hii iko katika njia ya Gorgan-Mashhad. Ninauhakika kuwa utafurahia tafrija hapo.
Mohammad: Mimi napenda mazingira. Hasa mandhari kama haya maridadi.
Romin:Baadhi ya wasafiri wanaopita njia hii, usiku wanakaa katika Bustani ya Golestan.
Mohammad: Basi sisi pia tuchukue hema na baadhi ya vitu vya dharura ili usiku tukae hapo.
@@@
Mwendeshaji: Sasa sikiliza mazungumzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.
@@@
Naam wapenzi wasikilizaji hapo ndio tunafika mwisho wa somo letu la 173 la Kifarsi. Unaweza kusikiliza kipindi hiki kupitia tovuti yetu ya http://kiswahili.irib.ir

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …