Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 12 Aprili 2012 17:22

Somo la Mia Moja na Sabiini na Mbili

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nasi katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 172 ambapo tutaangazia majirani wawili wa kaskazini mwa Iran ambao ni Jamhuri ya Turkmenistan na Jamhuri ya Armenia. Nchi hizi mbili zilipata uhuru mwaka 1991 baada ya kusamaratika shirikisho la sovieti. Watu wa Turkmenistan wanazungumza lugha ya Kiturkmani na waliowengi nchini humo ni Waislamu. Nao waliowengi nchini Armenia huzungumza kwa lugha ya Kiarmeni na ni wafuasi wa madhehebu ya kikristo ya Kiarmenia. Nchi Iran pia kuna jamii ya Warmenia. Turkmenistan na Armenia ni nchi mbili zenye historia na utamaduni wa pamoja na Iran. Leo Mohammad amekutana na Majid katika dhifa. Majid ni mfanya biashara ambaye huuza na kunuanua bodha na nchi jirani na Iran na amerejea hivi karibuni kutoka Armenia na Turkmenistan. Mohammad anamuuliza kuhusu nchi hizo mbili. Kabla ya kusikiliza mazungumzo yao kwanza tujifunze misamiati ya leo:
@@@
Mimi nimesikia----hivi karibuni-----wewe umerejea----takribani----mwezi moja-----mimi sikiwepo----wapi----wewe ulikuwa umesafiri-----mimi nilikuwa nimeenda----wewe ulikuwa umeenda----Armenia----Turkmenistan-----Mkurugenzi----Shirika----Kibiashara----Safari----Safari ya Kikazi----Miaka mingapi------nchi =kwa wingi=----uhisiano wa kibuashara----nunua----uza----mabadilishano-----bidhaa-----wewe unakusudia-----kazi yako-----wewe unastawisha-----hadisasa----sisi tumefanikiwa-----sisi tutastawisha-----sisi tunataka kustawisha----biashara-----Kiturkmani-----Kiarmenia----vitu gani---wewe unauza nje----mazao-----kilimo-----bidhaa----vyakula-----za madini----wao wanakaribisha-----wewe unaingiza----sisi tunaingiza----pamba--- uzalishaji----ya juu----nakutakia mafanikio----
@@@
Sasa tusikilize mazungmzo ya Mohammad na Majid wakiwa katika dhifa. Tafadhali zingatia
Effect : ) ( صدای ظروف و گفتگوی مهمانان
Mohammad: Nimesikia kuwa umerejea Iran hivi karibuni?
Majid: Ndio. Takribani mwezi moja sikuwa Iran.
Mohammad: Ulikuwa umesafiri wapi?
Majid: Nilikuwa Armenia na Turkmenistan. Mimi ni mkurugenzi wa shirika la kibiashara.
Mohammad: Basi ulikuwa umeenda safari ya kikazi?
Majid: Ndio. Ni miaka kadhaa sasa ambapo shirika letu lina uhusiano wa kibiashara na Armenia na Turkmenistan. NIlikuwa nimeenda huko kununua na kuuza na mabadilishano ya bidhaa.
Mohammad: Unakusudia kustawisha kazi zako katika nchi hizo?
Majid: Ndio. Hadi sasa tumefanikiwa na tunataka kustawisha biashara yetu na Waturkmani na Warmenia.
Mohammad: Mnauza vitu gani katika nchi hiz?
Majid: Waturkamni na Warmenia wanapenda mazao ya kilimo na bidhaa za vyakula na baadhi ya bidhaa za kimadini Iran.
Mohammad: Nyinyi munanunua nini kutoka nchi hizo?
Majid: Kutoka Turkmenistan tunanunua pamba na kutoka Armenia pia tunanuanua bidhaa za kilimo na mifugo.
Mohammad: Ni vizuri sana. Nakutakia mafanikio.
@@@
Kwa mara nyingine sikiliza mazungumo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.
@@@
Naam na hadi hapo ndio tunafika mwisho wa kipindi chetu unaweza kututumia maoni yako kupitia anuani yetu ya email ambayo ni This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Kipindi hiki kinapatikana katika tovuti ya http://kiswahili.irib.ir

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …