Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 12 Aprili 2012 17:20

Somo la Mia Moja na Sabiini na Moja

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami tena katika kipindi kingine cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi.
Somo letu la leo ni la 171 na ni matumaini yetu kuwa utakuwa nasi hadi mwisho. Katika kipindi cha leo tutaangazia, Iraq, nchini inayopakana na Iran upanda wa magharibi. Iraq ni nchi yenye utamaduni wa Kale na hivi sasa ina idadi ya watu takribani milioni 30. Karibu asilimia 75 ya watu wake ni Waarabu, asilimia 20 ni Wakurdi na waliosalia ni Waturkmani, Waashuri na kaumu nyinginezo. Nukta ya kuzingatia kuhusu Iraq ni kuwa ina Harama takatifu kadhaa za Maimamu wa Nyumba ya Mtume SAW.
Haram hizo ziko Najaf, Karbala, Kadhimein na Samarra. Kila mwaka maelfu ya Wairani hutembelea haramu hizo kwa lengo la ziara. Watu wa Iran na Iraq wana nukta nyingi sawa za kihistoria, kiutamaduni na kidini.
Baadhi ya Wairaqi kama wale walio maeneo ya Kurdistan wanafahamu lugha ya Kifarsi. Kabla ya kusikiliza mazungumzo ya leo tujifunze misamiati muhimu itakayotumika katika. Tafadhali zingatia.
@@@
Safari----Iraq----Ilikuwaje?----Iliburudisha----Kiziara----nzuri sana-----Haram----kadhaa-----wajukuu----Mtume----Sisi tulizuru-----Nafasi yenu ilikuwa wazi-----ipi----mji----mlienda-----Najaf----Karbala-----Kadhimein-----Samarra-----Sisi tulienda----Arbil-----Sisi tulitembelea-----kwa ajili yangu----kidogo----kumbukumbu-----wakati wangu-----Ziyara----Hiyo ilikuwa ikipita-----athari-----Kihistoria-----hewa----sana-----joto-----hasa-----wakati-----Adhuhuri----kwa kawaida-----magharibi----hoteli----sisi tungebaki----Kurdistan-----baridi-----laini-----vipi----kaskazini----nchi----eneo-----maeneo-----milima-----wastani----hiyo iko-----kilimo-----kustawi-----kijani kibichiii----baina-----mto----Dajla----Furat-----shamba-----bustani----- kuna----aghalabu-----mazao-----ni nini----tende----tamu----anuai
@@@
Sasa tusikilize mazungumzo ya Mohammad na Romin ambaye hivi karibuni amerejea kutoka safari Iraq. Wanafanya mazungumzo hayo wakiwa katika bustani moja ya Tehran
Effect: ) ( سر و صدای کودکان در پارک )
Mohammad: Safari Iraq ilikuwaje, ? ulifurahia?
Romin: Ndio. Safari ya kiziyara ni nzuri sana. Nilifanya ziara katika haram kadhaa za wajukuu wa Mtume SAW nchini Iraq. Nafasi yako ilikuwa wazi!
Mohammad: Ulienda miji ipi?
Romin: Nilienda Ziara katika miji ya Najaf, Karbala, Kadhimein na Samarra. Vile vile niliena Baghdad na Arbil.
Mohammad: Vizuri. Hebu nisimulie kidogo kumbukumbu za safari ya Iraq.
Romin: Katika miji ya Kiziara, wakati mwingi tulipitisha ziarani haram. Lakini pia tulitembelea athari za Kihistoria Baghdad na Arbil.
Mohammad: Hali ya hewa ilikuwaje?
Romin: Hali ya hewa ilikuwa joto sana hasa wakati wa adhuhuri. Kwa kawaida tulikaa hotelini kutoka adhuhuri hadi magharibi. Lakini hali ya hewa Arbil na Kurdistan ni baridi na tulivu.
Mohmmad: Vipi
Romin: Hii ni kwa sababu Kurdistan ya Iraq iko mashariki mwa nchi hii katika eneo la milima na wastani.
Mohammad: Je kilimo nchini Iraq kimestawi?
Romin: Ndio. Kurdistan iko katika eneo la kijani kibichi katika eneo lililo baina ya mito miwili ya Dijla na Furat na vile vile mashamba na mabustani mengi.
Mohammad: Aghalabu ya mazao ya kilimo Iraq ni nini?
Romin: Tende. Kuna tende tamnu na anuai nchini Iraq.
@@@
Mwendeshaji
Sikiliza tena mazungumzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili
@@@
Naam wapenzi wasikilizaji hadi hapo ndio tunafika mwisho wa kipindi chetu cha leo. Unaweza kusikiliza kipindi hiki katika tovuti yetu ya Kiswahili.irib.ir

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …