Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 11 Aprili 2012 15:13

Somo la Kwanza

Sikiliza
Mwendeshaji: Hamjambo Wapenzi wasikilizaji wa kipindi hiki kipya cha Jifunze Kifarsi. Nawakaribesha nyote kwa moyo mkunjufu kushiriki katika mfululizo wa vipindi vya Jifunze Kifarsi vya Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kama tulivyowajulisha katika kipindi kilichopita, Lugha ya Kifarsi ni lugha rasmi ya taifa ya Iran na moja ya lugha kongwe na tajiri zaidi duniani ambayo historia ya athari za maandishi yake inapindukia miaka zaidi ya elfu mbili. Kutokana na historia yake ndefu, lugha hii ina miundo miwili tafauti. Muundo wa kwanza ni ule ujulikanao kama Kifarsi cha Mazungumzo. Muundo wa pili ni wa Kifarsi cha Maandishi ambacho hutumiwa katika kusoma na kuandika. Katika vipindi vyetu hivi, tutaanza kujifunza Kifarsi cha mazungumzo na baadaye utajifunza kwa kiwango fulani namna ya kusoma na kuandika Kifarsi.
Awali kabisa tutaarifisha watu au wahusika wawili yaani Ramin na Muhammad ambao ni wanafunzi katika chuo kikuu cha Tehran. Ramin ni Muirani na anasoma somo la Historia. Lakini Muhammad si Muirani, yeye ni mwanafunzi kutoka Kenya anayejifunza fasihi ya Lugha ya Kifarsi. Leo adhuhuri baada ya kumalizika masomo yao watakutana katika mkahawa wa chuo na kuketi katika meza ya chakula cha mchana ambapo huo utakuwa mwanzo wa urafiki baina yao na kwa hakika mwanzo wa darasa zetu za Jifunze Kifarsi. Je unataka kujua ni vipi watakavyokuwa marafiki? Basi sikiliza kwa makini maneno watakayotumia katika mazungumzo yao. Sikiliza kwa makini na jaribu kukariri na kuandika maneno hayo.
Hujambo-
Bwana- Wewe- wewe ni- raia wa kigeni - Muirani -Unatoka wapi?- Mimi - Mimi ni - Ndio - Jina - Jina lako - Nini -Muhammad- Ramin- Jina Langu ni Ramin- Kwaheri
Mwendeshaji: Sasa rudia tena maneno hayo; Sikiliza mazungumzo ya Mohammad na Ramin katika mkahawa wa Chuo Kikuu.
Ramin: Hujambo Bwana
Muhammad: Sijambo
Ramin: Je wewe ni raia wa kigeni?
Muhammad: Ndio mimi ni Mkenya - wewe ni Muirani?
Ramin: Naam, mimi ni Muirani
Muhammad: Jina lako ni nani?
Ramin: Jina langu ni Ramin - Jina lako nani?
Muhammad: Jina langu ni Muhammad

Mwendeshaji: Naam, umesikiliza mazungumzo ya Ramin na Muhammad. Sasa zingatia mazungumzo hayo kwa mara nyingine tena.
Mara hii utasikiliza mazungumzo hayo bila tarjumi, hivyo fanya bidii kukariri wewe mwenyewe.................

Mwendeshaji: Ramin na Mohammad wanazungumza. Baada ya kumaliza chakula chao wanaagana na kuondoka mkahawani: Muhammad anamwambia Ramin:
Muhammad: Kwaheri Bwana Ramin
Ramin: Kwaheri
Mwendeshaji: Sasa sikiliza bila tarjuma.

Wapenzi wasikilizaji, katika kipindi chetu cha leo umejifunza kuamkia, kuuliza jina la mwenzako na kuagana naye.
Hadi hapo ndio tumefika mwisho wa kipindi chetu cha leo. Natumai nyote mumefaidika. Basi msikose kujiunga nasi wiki ijayo katika kipindi kingine cha 'Jifunze Kifarsi'. Khuda Hafez

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …