Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 14 Machi 2012 22:20

Somo la Tisini na Nne

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji hasa wapendao kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Ni matumaini yangu kuwa munafuatilia vipindi hivi. Somo letu la leo ni la 94. Hali ya hewa mjini Tehran ni baridi kidogo na Mohammad huenda chuo kikuu karibu kila siku. Anajitayarisha kwa ajili ya mitihani ya mwisho wa muhula.
Siku mbili zilizopita alihisi kichwa kinamuuma sana hasa baada ya adhuhuri. Amemeza temba kadhaa za kutuliza maumivu lakini hali yake bado ni taabani. Hivyo anaamua kuenda katika kliniki iliyo karibu na bweni ili amuone dakari. Anampiga simu katika kliniki ya Dk. Ramadhani na sekretari aliyhapo anamfahamisha aje kumuona daktari majira ya saa 11 jioni. Mohammad anafika hapo kiliniki saa 11 na anapata wangonjwa wengine wawili. Baada ya dakika 20 anaingia chuma cha Daktari. Jiunge nasi basi tusikilize mazungmzo yao. Lakini kwanza tujifunze misamiati ya kipindi cha leo.
$$
Hujambo----Bi----karibu---keti----juzi----kichwa changu kinaniuma---kichwa changu kina kisunzi---hali ya kichefuchefu---mimi nina----kisulisuli----mdomo---mdomo wako----fungua---mimi ninaona---nione---ulimi au lugha----ulimi wako---uchungu wa moyo---moyo wangu unaniuma----toa ruhusa---shinikizo la damu----nitapima-----mimi ninataka kupima-----tafadhali----mkono wa vazi----weka juu----jicho----kawaida---pakiti moja---tembe----sharubatiشربت-sindanoآمپول---mimi nitakuandikia----ni bora zaidi----kipimo cha damu----fanya----una---pengine una---- mafuta katika damu----mimi nitapatia---mimi ninaweza kupatia----kesho asubuhi----kabla ya----staftahi----nenda---maabara---asante----jawabu----kipimi----awali----fursa---nitakuletea

$$
Sasa sikiliza mazungmzo ya Mohammad na Daktari

Effect: ( صداي باز شدن در )

Daktari: Hujambo. Karibu, keti. Nini kimefanyika?

Mohammad: Bi Daktari. Tokeo juzi kichwa changu kinaniuma. Nina hali ya kichefuchefu pia.

Daktari:Una kisulisuli pia?

Mohammad: Ndio baadhi ya wakati kichwa changu kina kisunzi.

Daktari: Funfua mdomo wako. Nione ulimi wako. Una maumivu ya moyo pia?

Mohammad: Hapan, moyo wangu hauniumi.

Daktari: Niruhusu nipime shinikizo lako la damu . Tafadhali inua mkono wa shati.

Mohammad: Sawa. Tayari. چَشم . بفرماييد .

Daktari (baada ya muda)-Shinikizo lako la damu ni la kawaida. Nitakuandikia pakiti moja ya tembo, sharabati moja na sindano mbili. Ni bora iwapo utachukua kipimo cha damu. Pengine una Mafuta katika damu.

Mohammad: Ni lini ninaweza kuchukua kipimo cha damu?

Daktari: Kesho asubuhi kabla ya staftahi nenda maabara.

Mohammad: Asante sana bi Daktari. Nitakuletea matokeo ya kipimo cha damu fursa ya awali.

$$
Kwa mara nyingine sikiliza mazungmzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.

$$
Baada ya kuagana na daktari Mohammad anaenda katika duka la dawa na baada ya kunuanua dawa anarejea katika bweni. Akiwa njiani anawaza kuhusu ugonjwa wa mafuta katika damu. Anatumai kuwa baada ya kipimo hatokuwa na ugonjwa wowote. Chuo kikuu kina hospitali yenye maabara ya kisasa kabisa ambayo hutoa huduma kwa wanachuo na wahadhiri. Matokeo ya kipimo cha damu yanatoka baada ya siku mbili. Jiunge nasi katika kipindi chetu kijacho ili tujue ni yapi yatakayojiri atakapompelekea daktari matokeo ya vipimo. Unaweza kusikiliza vipindi vya kujifunza lugha ya Kifarsi kupitia ukurasa wetu wa intaneti ambao ni http://kiswahili.irib.ir.
Kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …