Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 14 Machi 2012 22:18

Somo la Tisini na Tatu

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nasi katika kipindi hiki cha kujifunza lugha ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 93. Kama unavyokumbuka, Romin na Mohammad wako katika mji wa Nishapur. Wako katika Makaburi Makubwa ya Attar na Kamal al Molk na wanavutia na makaburi hayo ya kihistoria yaliyojengwa kwa usanifu majengo mahiri na wa kihistoria. Mohammad na Romin wanazumgmza kuhusu malengo wawili wakubwa Wairani yaani Farid ad-Din Attar na Omar Khayyam. Attar alikuwa kati ya wanaerfani na wasomi bingwa maarufu Wairani na aliuwa na wavamizi wa Kimoghuli katika uzeeni. Naye Khayyan alikuwa kati ya wanahisabati, wamafalaki na malenga maarufu zaidi wa Iran. Yeye ndiye aliyetayarisha kalenda ya Kiirani zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Kalenda hii hivi sasa ni kati ya kalenda sahihi zaidi duniani na kwa kweli wengi wanashangaa ni vipi iliweza kuratibiwa kwa ustadi huo bila kuwa na kosa lolote. Heu tusikilize mazungmzo ya Mohammad na Romin wakiwa katika dua moja la kuuza vitabu lililo katika bustani kandoni mwa makaburi hayo mawili. Kwanza tusikilize misamiati muhimu itakayotumika katika kipindi cha leo.
$$

Bustani----sana---maridadi----kaburi kubwaآرامگاه----Kamal al Molk---ya kuvutia kuona-----wajua?----mimi nina fikiri----mchoraji----wachoraji---ni sahihi?---bora zaidi----takribani----80----mwaka---iliyopita----aliaga dunia---mkaazi wa Nishapur----Kashan----Kashani----kijana----yeye alienda----kisha----kutoka hapo----Ulaya---mafunzo----yeye alikuja----Mkurugenzi---Shule----Sanaa---Yeye alikuwaاو شد---kwa nini? ---mzeee---miaka ya uzeeni----umri---mwisho wa umri----hapa----kuishi-----yeye alikuwa akiishi----ubao (wa picha) تابلو ---ubao wa picha (kwa wingi)---jengo la makumbusho----majumba ya makumbusho----mbali mbali----Iran---kigeni----nchi za kigeni.
$$4
Tujiunge na Mohammad na Romin katika mazungmzo yao wakiwa katika bustani la kivutia huko Nishapur.

Mohammad: Bustani hili ni maridadi sana. Kaburi kubwa la Kamal al Molk pia linavutia kuliona.
Romin: Unamjua Kamal al Molk alikuwa nani?
Mohammad: Nafikiri alikuwa mchoraji. Ni sahihi?
Romin. Ndio. Alikuwa kati ya wachoraji bora zaidi wa Iran. Aliaga dunia takribani miaka 80 iliyopita.
Mohammad: Alikuwa mkaazi wa Nishapur?
Romin: Hapana. Kamal al Molk alikuwa wa Kashan. Akiwa kijana alienda Tehran na kisha kutoka hapo akaenda Ulaya.
Mohammad: Alienda Ulaya kwa ajili ya mafunzo ya uchoraji?
Romin: Ndio. Baadaye alikuja Iran na kuwa mkurugenzi wa shule moja ya sanaa.
Mohammad: Kwa nini kaburi lake liko Nishapur?
Romin: Kwa ajili katika miaka ya uzeeni, alikuja Nishapur na hadi mwisho wa umri wake aliishi hapa.
Romin: Michoro yake vile vile iko Nishapur?
Mohammad: Hapana: Michoro yake iko katika majumba ya makumbusho mbali mbali Iran na nchi za kigeni.

$$4
Kwa mara nyingine sikiliza tena mazungmzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.


###
Romin na Mohammad wanazungmza zaidi kumhusu Kamal al Molk na sanaa ya uchoraji nchini Iran. Baada ya adhuhuri wanaenda katika msikiti wa mbao. Msikiti huu ambao wote umejengwa kwa mbao kikamilifu ndio wa kwana kujengwa kwa mbinu hiyo duniani. Takribani tani 40 za mbao zimetumika kuujenga. Mohammad na Romin wanatembelea maeneo mengine ya Nishapur na wanapomaliza wanapanda treni kurejea Tehran. Ni safari yenye kumbukumbu nyingi kwa Mohammad. Ni matumaini yangu kuwa utapata fursa ya kuja Iran na kuutembelea mji wa Nishapur, mji wa Feruzi yenye kung'ara. Unaweza kusikiliza vipindi vya kujifunza lugha ya kifarsi katika ukurasa wetu wa intaneti ambao anuani yake ni http://kiswahili.irib.ir
Kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …