Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 14 Machi 2012 21:41

Somo la Tisini na Mbili

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji wapiendayo lugha ya Kifarsi. Karibuni kujiuna nasi katika somo letu la leo ambalo ni la 92. Kama munavyokumbuka, Mohammad na rafikiye Romin wamesafiri katika mji wa Nishapur. Wamefika katika mji huo ili kuutembelea Msikiti wa Jamia na soko la kale la Nishapur. Mji wa Nishapur ni mji wa malenga na wasomi bingwa. Kaburi kubwa la Attar, malenga na arif mkubwa wa Kiirani liko mjini Nishapur. Vile vile kaburi kubwa la Omar Khayyam, mwanahisabati na malenga maarufu wa Iran nalo pia liko mjini humo. Aidha mji huo una Maziara ya Wana wa Maimamu au Imamzadeh. Mji wa Nishapur ni mashuhuri huwa na hali nzuri ya hewa nyakati za asubuhi. Mohammad na Romin hivi sasa wakeo katika hoteli wakipata staftahi. Tusikilize mazungmzo yao lakini kwanza tujifunze misamiati muhimu itakayotumika katika kipini cha leo.

Sikiliza kwa makini
$$
Leo----Asubuhi----baridi kidogo---ya kupendeza---hewa----baridi---baadhi ya---Msafiri---Wasafiri---Wao wanabaki----wao wanapenda kubaki---kwa nini---kwa vile---wao wanafurahia----wao wanataka kufurahia---leo----sisi tunaenda----kaburi kubwa آرامگاه----kaburi la mwana wa Imamu امامزاده ---Attar---Khayyam----ni vizuri---Malenga----Muirani----mimi ninapenda----Kamal al Molk---Pale----baada ya adhuhuri----sisi tunaenda----wewe wapenda kuenda----Msikiti wa mbao----vizuri---ni vizuri----mahala au eneo---mahala ( kwa wingi)----ya kuvutia kuona----sana ---kale---kweli----kamera----kamera yako---film---wewe umenunua---mimi nitanunua.

####
Sasa sikiliza mazungmzo ya Mohammad na Romin wakiwa katika hoteli
Effect: در رستوران - صدای ظروف و همهمه مردم

Mohammad: Leo asubihi hali ya hewa ilikuwa baridi.
Romin: Ndio. Nyakati za Asubuhi Nishapur huwa baridi kidogo na hupendeza. Baadhi ya wasafiri hupenda kubakia Nishapur usiku.
Mohammad: Kwa nini?
Romin: Kwa vile hutaka kuburidika na hali ya hewa ya subuhi ya Nishapur.

Mohammad: Leo unaenda wapi?

Romin:Tutaenda Katika kaburi kubwa la Attari na la Khayyam

Mohammad: Vizuri sana. Mimi ninawapenda sana malenga hawa wawili Wairani.

Romin: Kaburi kubwa la Kamal al Molk na Kabur la mwana wa Imamu liko hapo pia.

Mohammad: Unafanya kazi gani baada ya adhuhuri?

Romin: Unapenda kuenda katika msikiti wa mbao?

Mohammad: Ni vizuri. Mji huo una maeneo mengi sana ya kujionea.
Romin: Kwa vile ni wa kale sana. Kweli, umenunua filamu ya kamera yako?

Mohammad: Hapana, leo nitanunua.
$$
Kwa mara nyingine sikiliza mazungmzo ya Mohammad na Romin lakini bila tafsiri ya Kiswahili.

$$
Mohammad anautembelea Msikiti wa Jamia na barabara za Nishapur. Na anapiga picha nyingi sana. Anapendezwa sana na usanifu majengo wa maeneo anayoyatembelea. Mji huo una mabustani megni ya kuvutia na Mohammad anafurahi sana kwa kupata fursa ya kuutembelea mji huu wa kuvutia na wa kihostoria. Mohammad na Romin Wamefika katika kaburi kubwa la Kamal al Molk lenye bustani kubwa na wanaanza kuzungmza. Basi usikose kusikiliza mazungmo yao katika kipindi chetu kijacho. Unaweza kusikiliza vipindi vya kujifunza lugha ya Kifarsi katika ukurasa wetu wa intaneti wenye anuani ya http://kiswahili.irib.ir. Kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …