Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 14 Machi 2012 21:37

Somo la Tisini na Moja

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na ni furaha yetu kuwa mumejiunga nasi katika sehemu nyingine ya kipindi cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 91. Katika kipindi hiki na viwili vitakavyofuata, tunataka kuwajulisha zaidi kuhusu mji wa kihistoria wa Nishabur Kaskazini Mashariki mwa Iran. Mji huu tokea zamani ulikuwa mkubwa na wenye umuhimu wa kiutamaduni kwa Iran. Wakati Wamoghul waliposhambulia Iran, Nishabur uliharibiwa sawa na miji mingine ya Mashariki mwa Iran. Maktaba yake iliyokuwa na takribani vitabu elfu moja iliteketezwa kabisa kwa moto. Mji huo una athari nyingi za Kihistoria. Pembizoni mwa mji huo kuna madini ya Feruzi ambalo ni jiwe lenye thamani kubwa na maridadi. Feruzi ya Nishabur ndiye bora na ghali zaidi duniani. Marafiki wawili, Mohammad na Romin wameamua kuutembelea mji huo. Wako ndani ya basin a wanazungmza kuhusu Nishabur. Kabla ya kusikiliza mazungmzo yao kwanza tujifunze misamiati muhimu ya kipindi cha leo. Sikiliza kwa makini.

Furaha---Basi (la abiria)---sisi tunasafiri----kijiji---vijiji----mahala---mahala (kwa wingi)---maridadi زيبا ---sisi tunaona----sisi tunaweza kuona----barabara---Tehran---Nishabur----kuzuri au maridadi قشنگ-Jangwa kidogo---Msikiti---Misikiti---Mgahawa---Migahawa---Sana---Mimi ninaona---ni sawa----kwa vile----Gari----Magari----Wao wanaondoka----njia----baada ya adhuhuri---sisi tutafika---takribani----saa---sisi tunaweza kuenda---soko----Msikiti wa Jamaa au Jamia---Kwa yakini---Hoteli---Mwanzo---Sisi tutapumzika---baada---sisi tutaenda----kidogo---sisi tutaenda matembezi----bora zaidi---hedaya---ni nini----jiwe----Feruzi----dunia---sana---ghali----kwa kiasi---rahisi----mimi ninapenda---petep---mimi nitanunua----mimi ninapenda kununia

****
Sasa tuwafuate Mohammad na Romin tupate kusikiliza mazungmzo yao.
Mohammad: Ninafurahi kuwa nina safiri kwa basi. Tunaweza kuona vijiji na maeneo maridadi.

Romin: Ndio. Barabara ya Tehran-Nishapur ni maridadi. Ni jangwa kidogo.

Mohammad: Ninaona Misikiti na Migahawa mingi katika Barbara hii.

Romin: Ni sawa. Kwa vile kuna magari mengi katika barabara hii, kuna misikiti na migahawa mingi njiani.

Mohammad: Tutawasilia Nishapur baada ya adhuhuri?

Romin: Ndio. Takribani saa tisa hivi.

Mohammad: Leo usiku tunaweza kuenda katika soko na Msikiti wa Jamaa wa Nishapur.?

Romin: Kwa yakini. Kwanza tutapumzika katika hoteli. Baadaye kwa ajili ya Sala tutaenda Msikiti wa Jamia kisha tutaembea kidogo katika soko.

Mohammad: Hedaya nzuri zaidi ya Nishapu ni nini?

Romin: Jiwe la Feruzi. Feruzi ya Nishabru ndio bora zaidi duniani.

Mohammad: Feruzi ni ghali mno?

Romin: Hapana. Jiwe hili la samawati ni maridadi sana, kwa kiasi ni rahishi.

Mohammad: Ninapenda sana kununua pete ya Feruzi.
###

Sikiliza tena mazungmzo ya Mohammad na Romin lakini bila tafsiri ya Kiswahili.

###
Mohammad na Romin, wanakula chakula cha mchana katika mgahawa moja pembeni mwa barabara ambapo watu wanapumzika. Hapo karibu kuna msikiti. Baada ya Kuswali na kula chakula dereva wa basi anawaita wasafiri wote ili waendelee na safari na wafike Nishapur baada ya adhuhuri. Wanapofika wanapumzika kisha wanaenda kuswali katika Msikiti wa Jamaa wa Nishapur ambao una vigaei vya Feruzi na bustani la kuvutia. Baada ya hapo wanaenda katika soko la kale. Lenye bidhaa nyingi. Wanatafuta pete za zikiwemo za Feruzi na Mohammad ananunua moja ya pete hizi. Mohammad anafahamu kuwa katika aghalabu ya mji ya Iran ina Msikiti wa Jamaa na soko pembizoni. Ni matumaini yangu kuwa utapata fursa ya kuja Iran na kuutembela mji wa kale wa Nishapur. Tunafikia tamati hapa kwa leo. Jiunge nasi katika somo letu lijalo na unaweza kusikiliza vipindi hivi katika ukurasa wetu wa Intaneti wa http://kiswahili.irib.ir.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …