Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 14 Machi 2012 17:38

Somo la Sabini

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nasi tena katika kipindi hiki cha kujifunza lugha ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 70 katika mfululizo huu.
Ni siku ya Jumapili na Mohammad anataka kuenda katika ubalozi wa nchi yake ulio hapa Tehran. Yuko ndani ya Taksi na kama kawaida barabara zina msongamano mkubwa. Dereva wa teksi anatumia njia za mkato kukwepa trafiki. Kwa mbali Mohammad anawaona watu wengi wakiwa wanaondoka kutoka katika jengo moja. Anazingatia kidogi na kugundua kuwa jengo hilo kubwa ni kanisa. Alikuwa hajawahi kufika katika barabara hii na kwa hivyo hakudhani kwamba kuna Wakristo wanaoishi Tehran na kwamba pia kuna makanisa katika mji huu. Dereva wa Taxi anapunguza kasi ya gari kwani kuna watu wengi wanaotaka kuvuka barabara. Hapo Mohammad anaanza kuzungmza na dereva wa Taksi.
Hebu tusikilize mazungumzo yao, lakini kwanza tujifunze misamiati muhimu ya kipindi cha leo. Tafadhali zingatia:
###
Hapa----Kanisa---Jumapili---Siku za Jumapili---Leo----Wao wanakuja---Mkristo----Wakristo----Fikiri----Mimi nilifikiri----pekee---Muislamu---Waislamu-----Waislamu wa Iran----Ishi----Wanaishi----Tehran----Yahudi----Mayahudi----Zartoshi----Mazartoshi----kweli راستي ---- Ipi----mji----miji----Yazd----Kermna----Isfahan----Urumiyeh----Shiraz----Ni vipi?----Ni sawa---Tabaan---idadi----ndogo----pekee----Shia----Ni Mashia----wengi----wengi wao----Sunni----Masunni---Mbali mbali-----rafiki---wao ni marafiki----sisi tupo---Iran----Kiirani----Bunge----Mbunge au mwakilishi----yote--- kundi---makundi----dini---kidini
... Sasa sikiliza mazungmzo hayo kwa makini.
Effect: ( صداي خيابان )
Mohammad: Hili hapa ni kanisa?
Dereva: Ndio. Hili ni kanisa. Leo ni Jumapili. Wakristo wa Tehran huja hapa siku za Jumapili.
Mohammad: Nilifikiri Waislamu tu ndio wanaoishi Tehran.
Dereva: Hapana. Katika Tehran, mbali na Waislamu kuna Wakristo, Mayahudi na Wazartoshi.
Mohammad: Je, Wazartoshi huishi katika miji ipi ya Iran?
Dereva: Katika Yazd, Kerman, Isfahan na Tehran.
Mohammad: Na Wakristo nao vipi? Wanaishi katika miji ipi ya Iran?
Dereva: Wakristo wanaishi Tehran, Isfahan na Urumiyeh.
Mohammad: Mayahudi vile vile wako Tehran?
Dereva: Ndio. Katika Tehran na Shiraza. Tabaan idadi yao ni ndogo.
Mohammad: Waislamu Iran ni Mashia pekee?
Dereva. Hapana. Wengi wao ni Mashia. Lakini Masunni pia wako na wanaishi katika miji mbali mbali ya Iran.
Mohammad: Wakristo, Mazartoshi na Mahahudi ni marafiki na Waislamu?
Dereva: Ndio: Sisi sote ni Wairani na ni marafiki.
Mohammad: Wao wana wawakilishi bungeni?
Dereva wa Taksi: Ndio: Makundi yote ya kidini Iran yana wawakilishi bungeni.
@@@
Mwendeshaji: Sikiliza tena mazungumzo ya Mohammad na Dereva wa Teksi lakini bila tafsiri ya Kiswahili.....
Dereva hapo anafafanua zaidi kuhusu namna waliowachache kidini wanavyopewa fursa ya kuwa na wawawakilishi katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran au Bunge. Vile vile wanaweza kufanya kazi katika idara za serikali na mashirika binafsi. Watoto wao pia wanarushusiwa kujifunza mafunzo ya dini zao na wana uhuru wa kuendesha shughuli zao za kidini. Nchini Iran makundi mengine yote ya kidini huishi pamoja kwa amani na Waislamu bila matatizo hata kidogo. Katika kipindi chote cha historia, hakujawahi kushuhudiwa vita vya kidini baina ya wafuasi wa dini mbali mbali nchini Iran. Ni matumaini yetu kuwa katika nchi yenu, sawa na hapa Iran, wafuasi wa dini mbali mbali wanaishi kwa amani na utulivu.
Tunafikia tamati hapa kwa leo, munaweza kuwasiliana nasi kupitia anuani yetu ya email ambayo ni This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. vile vile munaweza kusikiliza kupindi hiki kupitia mtandao wa intaneti kupitia Kiswahili.irib.ir hadi tutakapokutana tena, kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …