Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 11 Februari 2012 06:01

Somo la Mia Moja na Sabiini

Sikiliza
Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 170. Katika somo letu la leo tutaendelea kujifunza kuhusu nchi zinazopakana na Iran. Leo tutaangazia majirani wawili wa mashariki mwa Iran ambao ni Pakistan na Afghanistan.
Afghanistan iko mashariki mwa Iran na mji wake mkuu ni Kabul. Miji mingine muhimu ya Afghanistan ni Mazare Shariff, Jalal Abad na Kandahar. Kutokana na vita vya miaka mingi Afghanistan haijastawi sana kiuchumi. Lakini Waafghani ni watu wenye bidiisana. Lugha zao ni pamoja na Kifarsi, Kipashtu, Kiuezbeki na baadhi ya lugha nyinginezo. Nchi hiyo ya Kiislamu ina vyuo vikuu 13 na vyuo 6 vya waalimu. Nchi hiyo ina uhusiano mzuri wa kiuchumi na kisiasa na Iran. Pakistan iko kusini mwa Afghanistan na kusini mashariki mwa Iran. Mji mkuu wake ni Islamabad na mji mwingine mkubwa ni Karachi. Lugha rasmi ya nchi hiyo ni Urudu lakini lugha ya Kiingereza inatumika katika idara. Pakistan ni nchi ya sita kwa idadi ya watu wengi zaidi duniani. Na aghalabu ya raia wake ni Waislamu. Iqbal Lahore malenga mashuhuri wa Pakistan alizungumza pia kwa lugha ya Kifarsi na anaheshimiwa sana Pakistan na Iran. Leo Mohammad anazungumza na wanachuo wawili wa Pakistan na Afghanistan. Kabla ya kusikiliza mazungumzo yao tujifunze misamiati ya leo.
@@@
Kazi gani-----Iran nyini mumekuja------ufahamu-----shairi----Iqbal Lahore-----mimi ninataka kujifunza-------Lugha ya Kifarsi----Mtu wa----Afghanistan----Pakistan------Chuo Kikuu cha Tehran----Taaluma---Tiba------Mimi ninasoma------rafiki au kupenda-----bila shaka-----nyinyi mwajua-----zaidi-----watu Milioni 170---- idadi ya watu-----aghalabu ya watu------Waislamu------mwaka----hivi karibuni-----kujishughulisha------vita------kukaliwa kwa mabavu-----nchi-----kiasi gani-----idadi ya watu-----takwimu-----umoja wa mataifa------mwaka 2006----milioni 29-----watu----Pashtu----nyingine----wao wanazungumza------lugha rasmi------Kifarsi cha Kidari-----Kiutamaduni------historia----ya pamoja-----bila shaka-----uhusiano----kiuchumi-----kisiasa----tatu-----vizuri----kuelekea kustawi-----vivyo hivyo----kwa mfano-----uuzaji nje------sana------bidhaa-----vyakula----bidhaa za kiviwanda-----unaweza kupata.
@@@
Sasa sikiliza mazungumzo ya Mohammad na wanachuo wa Pakistan na Afghanistan wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Tehran. Tafadhali zingatia.
@@@
Mohammad: Nyinyi mumekuja Iran kufanya nini?
Taher: Ili kufahamu mashairi ya Iqbal Lahore nataka kujifunza lugha ya Kifarsi.
Yusuf: Mimi ni mwenyeji wa Afghanistan. Nasoma taalama ya udaktari katika chuo kikuu cha Tehran na ni rafikye Taher Ali.
Taher Ali: Bila shaka waijua Pakistan. Nchi yangi ina idadi ya watu zaidi ya 170 na waliowengi ni Waislamu.
Yusuf: Katika miaka ya hivi karibuni Afghanistan imetumbukia katika vita na kukaliwa kwa mabavu.
Mohammad: Nchi ya Afghanistan ina idadi ya watu kiasi gani.
Yusuf: Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa mwaka 2006, idadi ya watu katika nchi hii ni karibu milioni 29. Watu wa Afghanistan ni Waislamu na huzungumza lugha ya Kifarsi na Kipashtu na lugha nyingine kadhaa.
Mohammad: Je lugha rasmi ya nchi yako ni Kifarsi?
Ndio. Kifarsi cha Kidari na Kipashti ni lugha rasmi za Afghanistan.
Mohammad: Bila shaka nchi za Pakistan na Afghanistan zina historia ya utamaduni wa pamoja na Iran.
Taher Ali: Bila shaka., Uhusiano wa kiuchumi na kisiasa wa nchi hizi tatu ni mzuri sana na unastawi.
Yusuf: Ni vivyo hivyo. Kwa mfano Iran nje bidhaa zake Afghanistan. Unaweza kupata bidhaa nyingi za vyakula na kiviwanda vya Iran nchini Afghanistan.
@@@
Sasa sikiliza mazungumzo hayo kwa lugha ya kifarsi bila tafsiri ya Kiswahili.
@@@
Hadi hapo ndio tunafika mwisho wa kipindi chetu unaweza kusikiliza kipindi hiki katika tovuti yetu ya http://kiswahili.irib.ir

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …