Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 11 Februari 2012 06:00

Somo la Mia Moja na Tisiini

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nasi katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 190 na ndio somo la mwisho katika mfululizo huu. Mohammad ambaye amekuwa mhusika mkuu katika kipindi hiki ni mwanachuo ambaye amemaliza masomo katika taaluma ya lugha na fasihi ya Kifarsi katika Chuo Kikuu cha Tehran. Baada ya miaka mitano leo anaondoka Iran na kurejea nchi yake Kenya ambako ameazimia kufunza lugha ya Kifarsi. Marafiki zake wamekusanyika kwa lengo la kumuaga. Kila mmoja wao amemletea zawadi na Mohammad alikuwa hajatarajia hilo. Wote wamekuwa marafiki wa karibu wakati walipokuwa wakisoma pamoja katika Chuo Kikuu cha Tehran na wanakumbukumbu nzuri za kipindi hicho. Sasa hawana budi ila kutengana lakini urafiki wao utadumu. Wanaahidiana kuwa watakumbukana na kujuliana hali. Mohammad anarejea nchini Kenya lakini amezoea maisha Iran. Marafiki zake Mohammad hawamuachi hadi dakika ya mwisho akiwa Iran. Wamekuja kumsaidia kufunga mizigo yake. Rafiki yake wa Karibu, Romin anaandamana naye hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini ambapo wanaagana. Hebu tusikilize mazungumzo yao lakini kwanza tujifunze misamiati muhimu ya leo.
@@@
Kwaheri-----hisia-----ajabu-----ninafikiri-----ndugu yangu----tengana----hii hii-----hisia-----ninayo----bora zaidi------rafiki-----urafiki-----furaha----wewe wajua-----kwa ajili---watu-----mzuri----kujua-----wote----natumai-----wewe usisahau-----mimi nisahau----safari----wewe uwe na-----wewe ukifika-----upashe habari----bila shaka----azizi-----vitu vyote-----asante-----karibu----Mwenyezi Mungu mkarimu----mimi naacha-----kwa salama----kamwe----mahaba------kwaheri----
@@@
Sasa tusikilize mazungumzo ya Mohammad na Romin
Effect: افکت پرواز هواپیماها در فرودگاه
Mohammad: Hatimaye ni lazima tuagane.
Romin: Nina hisia za ajabu! Najihisi kama natengana na ndugu yangu.
Mohammad: Mimi pia nina hisia hiyo hiyo. Wewe ni rafiki yangu bora zaidi.
Romin: Mimi pia nina furaha kuwa urafiki nawe.
Mohammad: Wajua Romin! Mimi naipenda Iran kwa sababu ya watu wake wazuri na kujuana nawe na marafiki wengine.
Romin: Basi natumai kuwa hutatusahau.
Mohammad: Kweli yawezekana kuwasahau?
Romin: Natumai utakuwa na safari nzuri na utafanikiwa katika kazi zako.
Mohammad: Nashukuru. Mimi pia natumai utafikia malengo yako yote.
Romin: Wafikishie salamu baba na mama yako. Ukifika unakokwenda nipashe habari.
Mohammad: Bila shaka. Romin azizi, nakushukuru kwa yote.
Romin: Karibu. Nakuacha mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mkarimu. Nenda salama.
Mohammad: Kamwe sitasahau mahaba yako. Kwaheri.
@@@
Kwa mara nyingine sikiliza mazungumzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.
@@@
Naam wapenzi wasikilizaji, hadi hapo ndio tunafika mwisho wa mfululizo wa vipindi vyetu vya kujifunza lugha tamu ya kifarsi. Ni matumaini yetu kuwa mumeweza kufaidika na kipindi hiki kwa kujifunza Kifarsi na kuufahamu utamaduni na maisha ya watu wa Iran. Tunakutakieni mafanikio katika maisha na ni matumaini yetu kuwa tutakutana Iran panapo majaaliwa yake Mola.
Zaidi katika kategoria hii: Somo la Mia Moja na Themanini na Tisa »

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …