Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 11 Februari 2012 05:58

Somo la Mia Moja na Themanini na Tisa

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 189, tafadhali kuna nasi hadi mwisho.
Wafuatiliaji wa kipindi wiki wanamjua Mohammad ambaye amekuwa nasi katika vipindi vyetu vyote. Mohammad ni mwanachuo kutoka Kenya aliyekuja Iran kusoma taaluma ya Lugha na Fasihi ya Kifarsi. Amehitimu hivi karibuni katika taaluma hiyo na ameazimia kurejea nyumbani kwa lengo la kuanzisha Kituo cha Kujifunza Kifarsi. Katika kipindi chake chote cha masomo nchini Iran Mohammad alikuwa mwanachuo mwenye bidii sana. Alijifunza mengi sambamba na masomo yake ya kawaida ya chuo kikuu na hivyo yeye pia ni mtaalamu wa utamaduni na ustaarabu wa Iran. Hivi sasa anafuatilia masuala ya kiidara katika Idara ya Wanachuo wa Kigeni katika Chuo Kikuu cha Tehran. Akiwa hapo anakutana na mwanachuo wa kigeni ambaye karibuni hivi amekuja Iran kuendeleza masomo yake. Wanazungumza kuhusu masomo nchini Iran pamoja na maisha na utamaduni wa watu wa Iran.
Kabla hatujasilikiza mazungumzo yao tujifunze kwanza misamiati muhimu ya leo.
Kabla ya kusikiliza mazungumzo hayo, tujifunze misamiati muhimu ya leo.
@@@
Mwanachuo-----Kigeni-----samahani----Bwana-----kusajili-------mimi nimekuja-----chumba-----nambari 205-----orofa-----pili------mimi ninafikiri-----ofisi----Bi Ahmadi-----Wewe lazima uende-------miaka mitano-----Mimi ninasoma------darasa------Hizo zimemalizika-----imekuwa vizuri------mimi nimepata kujua------masomo------Chuo Kikuu-----ngumu----bila shaka-----rahisi-----si------mhadhiri------mzuri sana-----mtu----Utamaduni-----Kiirani------julikana----ni kwa sababu hii-----hofu-----wasi wasi----karimu----kukirimu wageni------maisha-----baina----uzoefu-----faida-----rafiki----Julikana-----siku ya kwanza-----hali-----mithili-----sasa-----mimi nina furaha-----mimi ninasikia------radhi----vitu vipya----wewe utajifunza-----nashukuru-----mimi nina matumaini---- wewe ufanikiwe-----
@@@
Effect ) ( صدای صحبت دانشجویان )
Sasa tusikilze mazungumzo ya Mohammad na mwanachuo wa kigeni
Mwanachuo wa Kigeni: Samahani Bwana. Nimekuja kujiandikisha. Chumba nambari 205 kiko ghorofa hii?
Mohammad: Hapana. Chumba hicho kiko ghorofa ya pili. Nafikiri wewe unapaswa kwenda ofisi ya Bi Ahmadi.
Mwanachuo:: Wewe ni mwanachuo wa kigeni?
Mohammad: Ndio. Ni miaka mitano sasa nasoma Iran na nimemaliza masomo.
Mwanachuo:.Ah. Ni vizuri kuwa nimekujua. Je, ni jambo gumu kusoma katika Chuo Kikuu cha Tehran?
Mohammad: Tab'an, si jambo rahisi. Lakini chuo hiki kina wahadhiri wazuri sana.
Mwanachuo: Mimi siwafahamu watu wa Iran na utamaduni wa Kiirani. Ni kwa sababu hii ndio maana nina wasi wasi kidogo.
Mohammad: Watu wa Iran ni wakarimu na huwakirimu wageni. Kuishi baina ya Wairani ni uzoefu wenye faida.
Mwanachuo: Lakini mimi sina rafiki wala simjui yeyote hapa.
Mohammad: Mimi pia katika siku ya kwanza nilikuwa na hali mithili yako. Lakini sasa nina marafiki wazuri nchini Iran.
Mwanachuo: Ninafuraha kusikia kuwa wageni wanaridhika na maisha na masomo nchini Iran.
Mohammad: Kila siku unajifunza vitu vupya hapa Iran.
Mwanachuo. Nashukuru. Ni matumaini yangu kuwa utapata mafanikio.
@@@
Mwendeshaji: Kwa mara nyingine sikiliza mazungumzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.
@@@
Wapenzi wasikilizaji hadi hapo ndio tunafika mwisho wa kipindi chetu cha leo

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …