Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 11 Februari 2012 05:57

Somo la Mia Moja na Themanini na Nane

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika kipindi hiki cha Jifunze Lugha ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 188. Ni matumaini yangu kuwa utakuwa nami hadi mwisho wa kipindi hiki.
Kama mnavyokumbuka, Mohammad alikuja Iran kuendeleza masomo yake ya juu. Sasa amefika mwisho wa muhula wa masomo yake. Kwa msaada wa wahadhiri wa chuo chake ameandika makala kuhusu mashairi ya Kiirani.
Amepanga kuitarjumu makala hii kwa lugha ya Kiswahili ili kwa njia hii awaarifishe malenga mashuhuri Wairani kama Ferdousi na Maoulavi kwa watu wa Kenya. Ferdowsi ni malenga wa karne ya nne Hijria au karne ya 10 Miladia na alitunga mashairi ya kitabu mashuhuri cha Shahnameh. Alijitahidi kuhuisha lugha ya Kifarsi kwa mashairi ya kihamasa na simulizi za kihistoria. Katika fasihi ya Iran, Ferdowsi anatambulika kama malengo mkubwa zaidi wa mashairi ya Kihamasa. Moulavi vilevile ni kati ya maurafa na malenga wakubwa wa karne ya saba Hijria au 13 Miladia. Mashairi yake aghalabu yalikuwa ya Kiirfani na masuala ya kirohoi.
Leo Mohammad na mhadhiri wake wanazungumza kuhusu malenga hawa wawili Wairani. Karibu kusikilizaj mazungumzo yao lakini kwanza tujifunze misamiati muhimu ya leo.
@@@
Mhadhiri----Nashukuru----Makala------wewe umesoma------wewe umesahihisha------ خواهش می کنم karibu-------makala-----maudhui----Ferdowsi------Andika-----Kubwa zaidi-------Malenga----Karne-----Nne Hijria sawa na Kumi Miladia-----mimi nimeandika----maisha-----pekee-----kughani mashairi-----sana----vizuri----Lugha ya Kifarsi----mara nyingine----hai -----bila shaka-----Moulavi----Malenga----kubwa au iliyojitokeza-----vivyo hivyo-----maalumu------ya kuvutia-----Shule au madrasa------Chuo Kikuu------Inafunzwa-----Fasihi-----Darasa-----pamoja------taaluma----mazingira-------ya masomo-----wanafunzi-------wanachuo-----Wao watajua----mimi napenda-----watu wa nchi yangu-----wao wajue----
@@@
Sasa tusikilize mazungumzo ya Mohammad na Mhadhiri wake.
Mohammad: Nashukuru mwalimu kuwa umesoma na kuisahihisha makala yangu.
Mhadhiri: Karibu. Katika makala hii andika mengi zaidi kuhusu Ferdowsi. Ferdowsi alikuwa malengo mkubwa zaidi katika karne ya nne Hijria.
Mohammad: Katika moja ya makala hizi nimeandika kuwa Ferdowsi alitumia muda wote wa maisha yake akitunga mashairi.
Mhadhiri: Vizuri sana. Ferdowsi alihuisha tena lugha ya Kifarsi.
Mohammad: Hapana shaka kwamba Moulavi vilevile alikuwa malenga mkubwa.
Mhadhiri: Sawa kabisa. Athari za Firdousi na Moulavi zinafahamika vyema duniani.
Mohammad: Ndio. Tarjumi ya baadhi ya mashairi yao yanapatikana katika nchi zingine.
Mhadhiri: Moulavi katika mashairi yake mazuri, ametoa uzingatiaji maalumu kwa mahaba na mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Mohammad: Ni jambo la kuvutia kuwa mashairi ya hawa malenga hufunzwa katika shule na vyuo vikuu.
Mhadhiri: Ndio, fasihi ya Kifarsi ni somo la pamoja na taaluma zote. Katika mazingira ya masomo, wanafunzi na wanachuo hujifunza mashairi ya malenga hawa wakubwa.
Mohammad: Mimi pia napenda watu wa nchi yangu wawajue malenga hawa wawili wakubwa.
@@@
Kwa mara nyingine sikiliza mazungumzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …