Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 11 Februari 2012 05:56

Somo la Mia Moja na Themanini na Saba

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kijiunga nami katika kipindi hiki cha kujifunza lugha tamu ya Kifarsi. Somo letu la leo ni la 187. Ni matumaini yangu kuwa utaendelea kuwa nasi hadi mwisho.
Romin anataka kuhudhuria hafla itakayoandaliwa na wanachuo. Kundi hili la wanachuo huandaa hafla za kidini katika minasaba mbalimbali. Romin na rafiki yake, Mohammad mwaka huu wamealikwa kushiriki katika hafla hiyo inayoandaliwa kwa munasaba wa Sikuu Kuu ya Idul Adha na Id Ghadir. Idi hizi mbili ni kati ya sikukuu muhimu ambazo kama zilivyo idi zingine za Kiislamu, huandaliwa kwa taadhima kubwa nchini Iran.
Kabla ya kusikiliza mazungumzo ya leo tujifunze kwanza misamiati muhimu itakayotumika.
Tafadhali zingatia.
Wewe wajua------keshokutwa-----likizo----idi----Adha----baadhi ya watu-----haswa-----wale walioenda----Hija---chinja------wao huchinja-----wewe utachinja-----baba----mwaka jana-----safari-----yeye alienda-----ishara----ucha Mungu------kujisalimisha-----mbele ya-----Mwenyezi Mungu-----mimi ninataka kushiriki----hafla-----wanachuo-------chuo kikuu-----wewe utakuja-----kwa kweli------sana-----mimi nina kazi-----lakini----napenda kushiriki------wiki ijayo-----Idi ya Ghadir----idi kwa wingi-----kubwa----Kiislamu-----mimi nitashirki-----sehemu zote----sherehe ya furaha------hiyo imeandaliwa-----vivyo hivyo-----watu-----Ahlul Bayt wa Mtume-----wao wanavutiwa-----
@@@@
Sasa sikiliza mazungumzo ya Romin na Mohammad.
@@@@
Romin: Mohammad wajua kesho kutwa ni likizo?
Mohammad: Ndio kesho kutwa ni Idul Adha.
Romin: Katika sikukuu ya Idul Adha baadhi ya watu hasa waliokwenda hija huchinja.
Mohammad: Nyinyi pia mtachinja?
Romin: Ndio. Baba yangu mwaka jana alienda safari ya Hija na siku ya idi atachinja.
Mohammad: Kuchinja mnyama katika siku ya Idi ni ishara ya ucha Mungu na kujisalimisha mbele ya Mwenyezi Mungu.
Romin: Mimi ninataka kushiriki katika hafla ya wanachuo wa Chuo Kikuu. Je wewe pia utakuja?
Mohammad: Kwa kweli nina kazi nyingi, lakini nataka kushiriki katika hafla hiyo.
Romin: Wiki ijayo pia ni sikukuu ya Ghadir. Idi ya Ghadir ni kati ya idi kubwa za Kiislamu.
Mohammad: Nitashiriki pia katika hafla ya Idi ya Ghadir.
Romin: Katika siku ya Ghadir hufanyika sherehe kote nchini Iran.
Mohammad: Sawakabisa. Watu wa Iran wanawapenda sana Ahlul Bayt wa Mtume SAW.
@@@
Kwa mara nyingine sikiliza tena mazungumzo hayo lakini bila tafsiri ya Kiswahili.
@@@
Na hadi hapo ndio tumefika mwisho wa kipindi cha kujifunza Kifarsi. Unaweza kutusikiliza kupitia tovuti ya Kiswahili.irib.ir

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …