Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 10 Novemba 2015 15:05

Ugaidi wa Kibiolojia, Ebola na Maslahi ya Marekani (2)

Ugaidi wa Kibiolojia, Ebola na Maslahi ya Marekani (2)

Virusi vya Ebola ambavyo vimekuwa vikitokea barani Afrika mara kwa mara ni virusi hatari vinavyoua aghlabu ya wagonjwa wake. Virusi hivyo viliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Virusi hivyo vilitokana na wanyama na vinaambukizwa kwa wanadamu kupitia damu na majimaji ya mwili au kugusa miili yenye virusi hivyo. Virusi hivyo haviambukizwi kwa njia ya hewa. Shirika la Afya Duniani (WHO) linaamini kuwa, kuna uwezekano mdogo sana wa kirusi cha Ebola kuambukizwa kupitia usafiri wa ndege. Pamoja na hayo wakati wa mgogoro wa virusi vya Ebola mashirika mengi ya ndege yalisimamisha safari zao katika nchi zilizoathiriwa na vurusi hivyo. Mwezi Machi mwaka 2014 kuliripotiwa kesi za kirusi cha Ebola katika nchi ya Guinea huko magharibi mwa Afrika. Virusi hivyo vilianza kuenea katika nchi nyingine za magharibi mwa Afrika na kuwakumba watu wengi katika nchi za Sierra Leone, na Liberia. Virusi hivyo pia viliingia katika nchi za Senegal na Nigeria ingawa viliweza kudhibitiwa haraka. Hadi kufikia tarehe 22 Oktoba mwaka 2014 zaidi ya watu elfu 10 walikumbwa na virusi hivyo na zaidi ya nusu yao waliaga dunia kutokana na maradhi hayo. Hadi Oktoba mwaka huo wa 2014 hakukuripotiwa kesi yoyote ya virusi vya Ebola nje ya bara la Afrika lakini mwezi huo huo wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani huko Uhispania na Marekani walipatwa na virusi hivyo wakati walipokuwa wakiwahudumia watu waliokumbwa na maradhi hayo.
Suala linayoyafanya maradhi ya virusi vya Ebola kuwa ya kipekee ni pamoja na kuenea kwake tu katika nchi za magharibi mwa Afrika, kusambaa katika nchi kadhaa kwa wakati mmoja, kusambaa zaidi mijini na kwa kasi kubwa ya kuambukizwa kwake. Kwa ujumla, baina ya mwaka 1976 wakati virusi vya Ebola vilipogunduliwa, hadi mwaka 2012 watu 2387 walikumbwa na maradhi hayo na 1590 miongoni mwao walifariki dunia katika maeneo ya mashariki mwa Afrika. Idadi ya watu waliopatwa na virusi vya Ebola mara hii ni mara nne zaidi ya mambukizi ya kabla yake. Maambukizi haya yamekuwa yakiongezeka maradafu kila mwezi. Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kilitathmini kuwa kama si uingiliaji zaidi au kama hakukufanyika mabadiliko ya mwenendo wa kijamii basi hadi kufikia Februari 2015 idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola katika nchi za Liberia na Sierra Leone ingefikia milioni 1.4. Hata hivyo kutokana na hatua zilizochukuliwa, kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo haukufikia kiwango hicho. Kwa mfano tu kufanyiwa marekebisho ada na taratibu za mazishi katika nchi ya Liberia kulisaidia kukusanyya karibu asilimia 85 ya maiti za watu waliofariki dunia kwa maradhi ya Ebola katika kipindi cha masaa 24 baada ya maafisa wa taifa kupashwa habari.
Agosti mwaka 2014 Shirika la Afya Duniani (WHO) lilikadiria kuwa karibu dola milioni 500 zinahitajika kwa ajili ya kudhibiti kasi ya maambukizi ya Ebola. Septemba mwaka 2014 taasisi za kimataifa zilizidisha kasi ya kukabiliana na Ebola. Umoja wa Mataifa ulianzisha taasisi ya kutoa radiamali ya haraka ya kukabiliana na virusi vya Ebola. Ilikaridiwa kuwa kunahitajika dola bilioni moja kwa ajili ya shughuli za taasisi hiyo.
Baadhi ya weledi wa masuala ya afya duniani wamekosoa radiamali ya Marekani na jamii ya kimataifa kuhusu ugonjwa wa Ebola na mwendo wa kinyonga na vilevile misaada kidogo ya nchi hizo katika uwanja huo. Hadi sasa bado kuna mjadala mkubwa juu ya suala kwamba Shirika la Afya Duniani linapaswa kuwa na timu ya radiamali ya haraka ya wataalamu wa afya kwa ajili ya kushughulikia matatizo makubwa ya kiafya kama virusi vya Ebola huko magharibi mwa Afrika.
Jumuiya ya misaada ya kibinadamu ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) inasema: "Kutochukuliwa hatua za dharura katika upeo wa kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Ebola kumekuwa na matokeo ya kusikitisha sana." Baada ya kupitia matukio ya mwaka 2014 jumuiya hiyo imesema kuwa nchi zilizopatwa na maradhi hayo na shirika la WHO hazikutilia maanani matakwa ya MSF.
Mhanga wa kwanza wa virusi vya Ebola alikuwa mtoto mdogo aliyefariki dunia Disemba mwaka 2013 nchini Guinea. Miezi mitatu baadaye yaani mwezi Machi mwaka 2014 Shirika la Afya Duniani lilitangaza rasmi habari ya maambukizi ya virusi vya Ebola na mwezi Agosti mwaka huo huo likatangaza hali ya hatari kote duniani. Hadi wakati huo watu elfu moja walikuwa tayari wamefariki dunia kutokana na maradhi ya Ebola na mwezi Oktoba idadi ya watu wlioaga dunia ilikuwa mara tano zaidi. WHO inasema japokuwa kesi za maambukizi ya Ebola zimepungua katika baadhi ya nchi lakini takwimu jumla za kuanzia mwezi Januari mwaka huu hazijapungua sana.
Wataalamu wanasema kuwa wametengeneza chanjo inayoweza kuwakinga panya dhidi ya aina hatari zaidi ya virusi vya Ebola. Watafiti wanasema hiyo ni chanjo ya kwanza ya virusi vya Ebola ambayo inaweza kutoa kinga ya muda mrefu dhidi ya virusi hivyo. Chanjo hiyo pia inaweza kuhifadhiwa kwa kipindi kirefu. Chanjo zilizotengeneza hapo habla hazikuwa na uwezo wa kuhifadhiwa kwa muda mrefu na zilikuwa zikipoteza taathira yake katika kipindi hicho. Hata hivyo watafiti wa Chuo Kiku cha Arizona nchini Marekani wametengeneza chanjo mpya yenye protini ya kutengeneza viwandani ambayo inachochea mfumo wa ulinzi wa mwili kwa ajili ya kutambua vyema kirusi cha Ebola na inafanya kazi vizuri baada ya kuhifadhiwa kwa kipindi kirefu.
Kuhusu chanzo cha virusi vya Ebola kumetolewa nadharia nyingine. Leonard J. Horowitz ameandika katika kitabu cha Sensitive Area ambacho ni miongoni mwa vitabu vilivyonunuliwa kwa wingi mjini New York kwamba: Marekani ilitengeneza virusi vya Ebola kwa shabaha ya kulinda eti usalama wake wa kitaifa na Israel na vilevile waitifaki wake wa zamani barani Afrika ikiwemo Afrika Kusini.
Kama tutatilia maanani mtazamo huu itatupasa kufanya uchunguzi wa Ebola barani Afrika na malengo ya Marekani katika kueneza na kusambaza virusi hivyo. Marekani imekuwa ikutumia silaha nyingine za biolojia kama kirusi cha kimeta (anthrax) katika baadhi ya nchi duniani. Suala hilo linaonesha mwelekeo mpya wa mipango ya Marekani ya kuingia katika nedani mpya ya ugaidi na mauaji ya kutumia silaha za biolojia.
Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza na yanayotokana na vijidudumaradhi (bacteria) wanasema kuwa virusi vya Ebola ni moja ya vimelea vilivyofanyiwa mabadiliko ya kijeni (GMO) ambavyo vilitengenezwa na kampuni ya masuala ya kijeshi ya Marekani kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Gazeti la Daily Observer ambalo ndilo kubwa zaidi nchin Liberia limechapisha ushahidi wa kisayansi na kuthibitisha kuwa Marekani ndiyo iliyotengeneza kirusi cha Ebola. Gazeti hilo limechapisha makala ya Professor Cyril Broderick akisema: Marekani inatumia virusi vya Ebola kama silaha ya biolojia kwa sababu vinaenea kwa kasi na vinaua akthari ya wahanga wake; na vilevile mtu anayemiliki chanjo yake anaweza kuwatwisha watu wengine matakwa yake.
John Presley ambaye ni miongoni mwa madaktari walioko kwenye kambi ya kupambana na Ebola nchini Sierra Leone anaashiri hatua ya kampuni ya Mapp ya Marekani ya kuzindua chanjo isiyo rasmi ya ya ZMapp dhidi ya virusi vya Ebola na kusema: Katika wimbi kubwa la propaganda vyombo vya habari vya Marekani kwanza vinazusha wasiwasi mkubwa kuhusu virusi hivyo kisha vinaashiria tiba yake, kama vilivyofanya wakati wa maambukizi ya virusi vya mafua ya ndege. Anaendelea kusema kuwa: Hii ni mbinu isiyo ya kibinadamu wala ya kimaadili ya Wamarekani ambayo imenyaziwa kimya na jamii ya kimataifa.
Dakta Francis Boyle wa Chuo Kikuu cha Illinois nchini Marekani amekanusha madai yanayosema kuwa virusi vya Ebola ni matokeo ya mgogoro wa usafi na masuala ya afya barani Afrika akisema maneno hayo ni propaganda tupu. Msomi huyo anaendela kusema: Kwa mujibu wa utafiti waliofanya wao Ebola ni matokeo ya vita vya kibiolojia na kwamba vilitengenezwa katika maabara za Marekani katika pwani ya magharibi mwa Afrika.

 

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …