Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Machi 2013 18:27

Matatizo ya Familia katika nchi za Magharibi (14)

Matatizo ya Familia katika nchi za Magharibi (14)

Hamjambo wasikilizaji wapenzi na karibuni kuwa name tena katika mfululizo wa makala hizi zinazozungumzia mgogoro wa familia katika nchi za Magharibi. Katika zana za sasa zil;izopewa zama za mawasiliano, vyombo vya habari kama magazeti, intaneti, redio, televisheni na kadhalika vimekuwa na taathira kubwa kwa taasisi ya familia. Bidhaa za kiutamaduni ambazo licha ya kuwa na faida nyingi za kimafunzo, kimalezi, kisanaa na burudami kwa mwanadamu lakini pia zimezusha matatizo mengi ya kijamii. Katika kipindi chetu hiki ambacho ni cha 14 cha mfululizo huu tutatupia jicho walau kwa muhtasari taathira a vyombo vya mawasiliamo ya umma kwa familia. Tafadhali endeleeni kuwa kando ya redi zenu kusikiliza niliyokuandalieni kwa leo. 

XXXX

Katika zama hii familia inakabiliwa na mabadiliko makubwa. Masuala kama kupungua idadi ya watoto, kubadilika nafasi ya mke na mume ndani ya familia na katika jamiina sababu nyinghine za kijamii vimebadilisha muundo wa familia za zama hizi. Bidhaa na vipindi cha redio na televisheni, kanali za televisheni za satalaiti, mtandao wa intaneti, vitabu, magazeti na majarida vimekuwa na taathira kubwa mno katika malezi ya watoto na masuala yanayohusiana na familia.

Ni vyema kusema hapa kuwa familia ina nafasi kubwa na muhiumu sana katika malezi ya watoto. Kwani kwa hakika mwanadamu huanza kupata na kujifunza itikadi za kidini, utamaduni, ada na desturi ndani ya familia yake. Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi uliofanyinwa na Kaiser Family Foundation huko Marekani mwaka 2005 vijana wenye umri wa kati ya miaka 8 hadi 18 kwa wastani hulengwa wkas hujuma za vyombo vya habari masaa 5.6 kwa siku na kwamba runinga ina hisa kubwa zaidi katika hujuma hiyo.

Mwandishi na mnadharia wa Kimarekani Neil Postman ni miongoni mwa wasomi waliotumia sehemu kubwa ya umri wao kuweka wazi na kukosoa vyombo vya habari hususan televisheni nchini Marekani. Msomi huyo anasisistiza katika kitabu alichokipa jina la "Kujiburudisha Hadi Kifo" akisisitiza kuwa: Kughiriki watoto katika anga ya vyombo vya habari kunaweza kuwa na madhara makubwa kwao na jamii watakayoijenga hapo baadaye. Kwa msingi huo msomi huyo hufadhilisha kuzima televisheni kwa muda mwingi.

Kwa sasa televisheni imekuwa sawa na mwanachama wa familia zetu. Kwani mbali na kurusha hewani matanfgazo na vipindi vyake hutumia mbinu tata na za kisaikolojia kwa ajili ya kupenya ndani ya fikra za waliowengi katika jamii. Kiboksi hicho cha uchawi kinaweza kutayarisha uwanja mzuri wa ustawi na maendeleo iwapo kitatumiwa kupasha habari na kuelimisha jamii kwa njia sahihi. Vivyo hivyo redio, ina nafasi na mchango mkubwa katika masuala ya kijamii na kustawisha vipawa vya vijana na mabarobaro. Sisi sote tunaelewa kwamba macho na masikio ya vijana yanapenda sana kudadisi na kujua mambo na huwa mithili ya darubini ambayo huzunguka huku na kule kuchukua picha za mandhari zote. Macho na masikio ya vijana huwinda kwa umakini mkubwa mandhari zote ndani ya filamu za kimapenzi, michezo ya televisheni, matangazo ya biashara na hata maneno yanayosemwa katika nyimbo mbalimbali. Tunaweza kusema darubini za macho ya watoto na vijana hayakosi kusajili na kupiga picha hata harakati ndogo kabisa zisizokuwa za kawaida katika filamu kama hizo.

Hapana shaka kuwa kutumia bidhaa zisizo sahihi za kiutamaduni huangamiza vipawa vya vijana na kupunguza uwezo wao wa ubunifu.

Mwandishi Mary Winn wa Marekani anasema vyombo vya sasa vya habari huwafanya watoto kuwa tegemezi na kupunguza hamu yao ya kuvumbua vipawa vyao na kutaka kujitegemea. Tofauti kabila na usomaji kitabu ambako wataalamu wanasema kuwa huzidisha umahiri wa mtoto na kuboresha uwezo wake.

Hii leo matangazo na vipindi vingi vya redio na televisheni vinaweza kufanya mabadiliko makubwa katika masuala ya kiutamaduni na kijamii. Dakta Sharifi ambaye ni mwanachama wa kituo cha utafiti wa masuala ya Familia nchini Iran anasema kuwa katika miaka ya huko nyuma watu wa familia walikuwa wakiishi pamoja kwa maana halisi ya neno hilo. Hata hivyo, anasema Dakta Sharifi, kudhihiri masuala kama televisheni ni miongoni wma mambo yaliyogawa na kusambaratisha misingi ya familia. Anaongeza kuwa si tu kwamba televisheni imekua na taathira katika utamaduni, thamani za kaumu mbalimbali na masuala mengine mengi bali pia imekuwa na taathira kubwa katika masuala madogomadogo ya maisha ya kila siku kama jinsi ya kuket na kusimama watu a ndani ya familia moja. Moja ya taathira mbaya za vipindi vya televisheni ni kupunguza uhusiano wa upendo baina ya baba, mama na watoto wao. Anasema kuwa suala hilo linashuhudiwa zaidi katika miji mikubwa.

Kutokana na taathira hiyo kubwa ya vipindi vya runinga katika maisha ya kila siku ya watu, mfumo wa ubepari unatumia chombo hicho kwa ajili ya kubadili tabia na hata ada na mahitaji halisi ya kaumu mbalimbali. Kwa mfano mfumo wa kibepari unaweza kuwaelekeza watu wa jamii moja katika bidhaa fulani wka kutumia nguvu na taathira ya vipindi na matangazo ya televisheni na redio na kutengeneza faidi kubwa ya fedha kwa ajili ya makampuni makubwa ya Kimagharibi. Kwa utaratibu huo gharama za matumizi ya familia hupanda juu suala ambalo huwa kikwazo na tatizo wka vijana wanaotaka kuanzisha familia zao wenyewe.

Miongoni mwa taathira mbaya za vyombo vya habari ni ongezeko kubwa la ukatili na vitendo vya utumiaji mabavu kati ya kizazi cha vijana. Uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa vyombo vya mawasiliano ya umma vina mchango mkubwa katika kueneza ukatili na vitendo vya kutumia mabavu. Filamu na vipindi vya televisheni vinavyoonesha matukio ya kikatili na jinai zinazidisha sana moyo wa kupenda ukatili na kutenda jinai kwa watu wanaotazama vipindi hivyo. Wakati huo huo wataalamu wa elimu jamii wanaamini kuwa watoto wanaoshuhudia ukatili unaofanywa na mzazi mmoja dhidi ya mwenzake au filamu za kikatili na vitendo vya uhalifu na jinai huwa na mienendo ya kupenda kutumia mabavu na ukatili. Hii ni kutokana na ukweli kwamba vyombo vya mawasiliano ya umma vinavyotangaza na kuonesha filamu na vipindi kama hivyo wka hakika huwa vinatoa ujumbe kwamba kufanyika kwa vitendo kama hivyo ni jambo la kawaida na hivyo kuwafanya watoto na vijana waelewe kuwa si jambo baya mambo kama hayo kutokea katika jamii au familia zao.

Kwa mfano tu mauaji yaliyotokea katika shule ya Columbine huko Marekani yameonesha ni kwa kiasi gani kijana mdogo wa shule alivyoathiriwa na filamu za matukio ya kikatili na utumiaji mabavu zinazoonyeshwa katika televisheni nchini humo. Wanafunzi wawili Columbine High School waliwaua kwa kuwamiminia risasi ya wanafunzi wenzao 12 na mwalimu mmoja wakiigiza filamu za action. Mauaji kama haya yanakariri mara kwa mara nchini Marekani.

Filamu za matukio ya kikatili na zile zinazojaa ufuska na ngono huwaathiri haraka sana vijana kwa kadiri kwamba hujaribu kuiga yale wanayoyaona katika vipindi na filamu hizo.

XXXX

Wapenzi wasikilizaji, muda uliotengwa kwa ajili ya kipindi hiki unaekela ukingoni. Sina budi kuishia hapa kwa leo nikiwa na matumaini ya kukutana tena nanyi wiki ijayo panapo majaaliwa na Mola Muumba. Kwaherini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)