Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 19 Oktoba 2014 09:36

WHO: Ebola inazidi kuongezeka katika bara la Afrika

WHO: Ebola inazidi kuongezeka katika bara la Afrika

Tarik Jasarevic Msemaji wa Shirika la Afya Duniani WHO amesema kuwa, ukosefu wa suhula za tiba na hospitali ni miongoni mwa sababu zinazochangia  kuongezeka maradufu waathirika wa homa ya Ebola ikilinganishwa na miezi iliyopita. Msemaji wa WHO ameyasema hayo baada ya kuzitembelea nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia ambazo zimekumbwa na maradhi ya Ebola na kusisitiza kwamba, kila mwezi idadi ya waathirika wa homa ya Ebola huongezeka maradufu katika nchi hizo. Jasarevic ameongeza kuwa, ukosefu wa suhula muhimu kama vile vitanda kwenye mahospitali na kwenye vituo vya uangalizi maalumu, ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka wagonjwa wa Ebola kila mwezi. Msemaji wa Shirika la Afya Duniani amesema kuwa, kuendelea kubaki waathirika wa Ebola kwenye familia, kumechangia pia kuongezeka kasi ya ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa haujapatiwa tiba wala chanjo. Jasarevic amebainisha kuwa, hadi sasa jumla ya watu 4,555 wameshafariki dunia na wengine 9,216 wameshaambukizwa maradhi ya Ebola katika nchi kadhaa duniani  na hasa katika eneo la magharibi mwa Afrika. 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …