Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 24 Septemba 2014 19:00

Wahanga wa Ebola huenda wakafikia milioni 1.4

Wahanga wa Ebola huenda wakafikia milioni 1.4

Shirika moja kubwa la afya la Marekani limetoa ripoti likitabiri kwamba, watu wapatao milioni 1.4 huenda wakakumbwa na virusi vya Ebola ifikapo mwezi Januari mwakani kama hatua za haraka hazitachukuliwa kupambana na ugonjwa huo.
Shirika hilo la afya la CDC limesema katika ripoti yake ya kila wiki iliyotolewa jana kwamba, kama hatua za haraka hazitachukuliwa, basi watu wapatao milioni 1.4 watakuwa wameambukizwa ugonjwa wa ebola ifikapo Januari 20 mwakani.
Ripoti hiyo imetolewa muda mchache baada ya kutolewa ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO iliyozungumzia kuongezeka vibaya maambukizi ya ugonjwa huo hatari huko magharibi mwa Afrika.
Itakumbukwa kuwa, kuanzia tarehe 19 Septemba mwaka huu, idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa huo katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone imeongezeka mno na kufikia watu 5,843, huku watu wapatao 2,800 wakiwa wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …