Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 19 Agosti 2014 09:33

WHO: Wasafiri wachunguzwe homa ya Ebola

WHO: Wasafiri wachunguzwe homa ya Ebola

Shirika la Afya Duniani (WHO) limezitaka nchi za magharibi mwa Afrika zilizoathiriwa na ugonjwa wa Ebola kuwachunguza wasafiri wote katika viwanja vya ndege vya kimataifa, bandari na vivuko vikubwa vya nchi kavu ili kuzuia kuenea zaidi ugonjwa huo.
WHO imesema kuwa, maafisa wa nchi wanapaswa kumzuia kusafiri mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa huo, isipokuwa kama safari hiyo ni sehemu ya uchunguzi wa kitiba. Hayo yanajiri huku Cameroon ikifunga mipaka yake yote ya nchi kavu, bahari na anga na Nigeria, hatua iliyochukuliwa ili kuzuia kuenea virusi vya homa ya Ebola, ijapokuwa bado hakujahushudiwa mgonjwa wa Ebola nchini Cameroon.
Wakati huo huo maafisa wa Liberia wanaendelea kuwatafuta wagonjwa 17 wa Ebola waliotoroka katika zahati iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya waathirika wa ugonjwa huo baada ya kituo hicho kuvamiwa na watu waliokuwa na silaha. Waziri wa Afya wa Liberia amesema kwamba, wagonjwa hao bado hawajulikani walipo na kwamba waporaji waliovamia zahanati hiyo walipora matandiko na vifaa vingine vilivyokuwa vikitumiwa na wagonjwa.
Watu zaidi ya 400 wamefariki dunia kutokana na homa ya Ebola nchini Liberia.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …