Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 31 Disemba 2014 20:29

Uwezo wa kijeshi Iran, chimbuko la utulivu kieneo + Video

Rais Rouhani akikagua gwaride ya meli na ndege za kivita kusini mwa Iran Dec. 31 2014 Rais Rouhani akikagua gwaride ya meli na ndege za kivita kusini mwa Iran Dec. 31 2014

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nguvu na uwezo wa vikosi vya ulinzi vya jeshi la Iran si tu kwa ajili ya nchi hii bali pia ni chanzo cha utulivu na usalama kwa nchi za eneo la Mashariki ya Kati.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika bandari ya Jask kusini mwa Iran wakati alipohudhuria gwaride kubwa ya meli na ndege za kivita za Iran wakati wa kumalizika mazoezi ya vikosi vya majeshi ya nchi. Rais Rouhani ameongeza kuwa vikosi vya jeshi la Iran vimeweza kuimarika na kupata nguvu licha ya kuwa nchi hii imewekewa vikwazo kwa zaidi ya miaka 35 sasa. Rais wa Iran amesema majeshi ya nchi hii hayana nia ya kuhujumu nchi yoyote ile bali lengo lake ni kujihami.

Jeshi la Iran lilianzisha mazoezi hayo Desemba 25. Katika mazoezi hayo yaliyopewa jina la 'Muhammad Rasulullah SAW' , Jeshi la Iran limetumia meli za kivita, nyambizi, makombora, ndege za kivita, ndege zisizo na rubani na helikopta.  Aidha aina mbalimbali ya silaha zimefanyiwa majaribio katika mazoezi hayo. Mazoezi hayo yalifanyika katika eneo lenye upana wa kilomita mraba milioni 2.2, kuanzia mashariki mwa Lango Bahari la Hormuz katika Ghuba ya Uajemi hadi kaskazini mwa Bahari ya Hindi na maeneo ya kusini mwa Ghuba ya Aden katika Pembe ya Afrika.  

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayari amesema mazoezi hayo ya siku sita mbali na kuonyesha uwezo wa kijeshi nchini yalilenga kunyoosha mkono wa amani na urafiki kwa msingi wa umoja wa Waislamu na umoja katika eneo hili.  

Ingia katika video hii hapa chini kuangalia sehemu ndogo tu ya uwezo wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

 

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)