Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 28 Disemba 2014 19:39

Marekani yakimbiza meli baada ya kuonywa na Iran + Video

Marekani yakimbiza meli  baada ya kuonywa na Iran + Video

Meli za kigeni ikiwemo manuwari ya kivita ya Marekani zimelazimika kuondoka kwenye eneo la manuva ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanayojulikana kwa jina la Muhammad Rasulullah SAW baada ya kuonywa na wanajeshi wa Iran. Habari kutoka kwenye luteka hiyo ya kijeshi zinasema kuwa, ndege moja ya kivita ya Iran iliyokuwa inapiga doria kwenye eneo la mazoezi hayo ya kijeshi leo Jumapili iligundua meli za kigeni ikiwemo manuwari ya kivita ya Marekani zikiwa zimeingia katika masafa yaliyoainishwa kwa ajili ya kufyatulia makombora ya Iran na ikatoa onyo kwa meli hizo za kigeni kuondoka mara moja kwenye eneo hilo nazo zimeondoka haraka bila ya kukaidi amri hiyo. Kabla ya hapo, Admeli Habibollah Sayari, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikuwa ametangaza kuwa, tayari Iran imeainisha masafa ambayo yatakuwa yanafika makombora yake katika mazoezi hayo ya kijeshi. Alisema: Tumewaonya wageni waondoe vyombo vyao kwenye masafa hayo. Alisema, jambo hilo limefanyika kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kwamba chombo chochote kitakachokaidi amri hiyo kitabeba chenyewe lawama za madhara yatakayotokea. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikitangaza mara kwa mara kuwa uwezo wake wa kijeshi si tishio kwa nchi nyengine na kusisitiza kwamba kanuni ya mfumo wake wa ulinzi inalenga kuzuia kitisho cha mashambulio ya kichokozi.

Ingia hapa chini kuangalia video ya tukio hilo

 

 

 

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)