Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 26 Disemba 2014 18:48

Ndege anayetumia mbinu ya ajabu kuvua samaki

Ndege anayetumia mbinu ya ajabu kuvua samaki

Video hii hapa chini inamuonesha ndege akitumia mbinu ya ajabu kuvua samaki. Hilo halitokani na chochote isipokuwa uwezo Mkubwa wa Allah aliyemuumba ndege huyu.

 *******

Kwa hakika ametukuka Mwenyezi Mungu Mtukufu Ambaye amemjaalia kila kiumbe njia yake ya kupatia rizki. Allah ana habari ya kila kitu. Hachukuliwi na usingizi wala kusinzia. Ni Msimamiaji wa kila kitu na ana elimu na kila kitu. Katika Suratul an Aam, aya ya 59, Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'ani Tukufu kwamba:

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لاَ يَعْلَمُهَا إِلاَّ هُوَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلاَّ يَعْلَمُهَا وَلاَ حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الأَرْضِ وَلاَ رَطْبٍ وَلاَ يَابِسٍ إِلاَّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ

Na ziko Kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilichoko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.

Amma kuhusu neema na rizki Zake kwa viumbe Mwenyezi Mungu anasema katika sura ya 11 ya Hud aya ya 6 kwamba:

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الأَرْضِ إِلاَّ عَلَى اللَّهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ

Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha.

Na katika aya ya 60 ya Suratul Ankabut, Qur'ani Tukufu inasema:

وَكَأَيِّن مِن دَابَّةٍ لا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

Na wanyama wangapi hawawezi kujimilikia riziki zao! Mwenyezi Mungu anawaruzuku hao na nyinyi pia. Na Yeye Ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.


Ingia kwenye video hii hapa chini kuona kipande hicho cha video ambacho kimetembelewa na watu wengi katika mitandao ya kijamii.

 

 

 

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)