Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 24 Novemba 2014 14:06

Ajali mbaya ya treni nchini Kazakhstan + Video

Ajali mbaya ya treni nchini Kazakhstan + Video

Hawakukosea waliosema, ajali haina kinga. Lori moja ambalo dereva wake anaonekana alishindwa kulisimamisha kutokana na barabara kuteleza wakati wa theluji kali, limepata ajali mbaya ya kugongwa na treni nchini Kazakhstan.
Katika video hii hapa chini, kamera ya barabarani imerekodi tukio hilo la kutisha ambalo linaonesha lori likija pole pole kutokea mbali kama ishara ya kwamba dereva alikuwa anajaribu kufunga breki, lakini likamshinda na kusimama pembeni kabisa mwa reli.
Treni lililokuwa linatokea upande wa kushoto halikuligusa lori hilo, lakini ghafla moja linaonekana treni likipita kwa kasi kutoka upande wa kulia na kulipiga kwa nguvu zote lori hilo, na kusababisha ajali mbaya hadi kwa treni la pili. Kwa mujibu wa ripoti, dereva wa lori hilo alikufa papo hapo.

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)