Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 12 Novemba 2014 20:44

Iran yazindua drone inayoshabihana na RQ-170 + Video

Iran yazindua drone inayoshabihana na RQ-170 + Video

Iran imezindua ndege yake isiyo na robani (drone) inayoshabihiana na ile ya Marekani iliyolazimishwa kutua Iran miaka mitatu iliyopita ambayo wataalamu Wairani wamefanikiwa kutengeneza bora zaidi yake.

‘Drone’ hiyo ya Iran inashabihiana na ile ya Marekani ya RQ-170 isiyoonekana kwenye rada. Itakumbukwa kuwa Disemba 4, 2011, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitumia maendeleo yake ya teknolojia ya vita vya kielektroniki na kuilazimisha kutua chini ndege ya kisasa ya kijasusi ya Marekani baada ya kuingia kwa siri katika anga ya Iran na kuichukuwa ngawira. Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH liilifanikiwa kupata taarifa zote zilizokuwemo kwenye ndege hiyo ya kijasusi. Baada ya uchunguzi wao wa kina, wahandisi wa Iran wamefanikiwa kuunda drone bora zaidi ya hiyo ya Marekani.

Baada ya kunaswa, Rais Barack Obama wa Marekani aliwaomba wakuu wa Iran wairejesha ndege hiyo ya kisasa kabisa lakini ombi lake lilipuuzwa jambo ambalo lilihesabiwa kuwa ni fedheha kubwa kwa Rais huyo wa Marekani.

Akizungumza wakati wa kuzinduliwa drone hiyo,  Brigedia Jenerali Amir-Ali Hajizadeh mkuu wa kitengo cha Anga za Mbali katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, ‘Mbali na uhandisi kinyume uliofanywa na wataalamu wa Iran katika wa ndege hii isiyo na rubani, pia ndani yake tumeweza kupata taarifa za siri ambazo ni muhimu zaidi ya ndege yenywe. Vile vile tumeweza kubaini mbinu ambazo Wamarekani walikuwa wakitumia kufanya ujasisi katika drone hii. Ndege hii tuliyotengeneza ni bora zaidi kuliko mshabaha wake kwani inatumie mafuta machache, pie tumeimarisha uwezo wake wa kukwepa rada.’

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)