Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 20 Agosti 2014 16:25

Waziri Amina Mohammed azungumza na Radio Tehran + Video

Waziri Amina Mohammed azungumza na Radio Tehran + Video

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Bi Amina Mohammad ambaye yuko katika ziara ya kikazi hapa mjini Tehran amezungumza na Idhaa ya Kiswahili, Radio Tehran kuhusu malengo ya safari yake.

Kama ambavyo amezungumza pia na waandishi wa mashirika mengine mbalimbali ya habari kuhusu masuala tofauti ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuimarishwa uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kenya katika nyanja zote.

Waziri Amina Mohammad pia amekutana na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa Iran pamoja na raia wa Kenya waliopo hapa mjini Tehran.

Katika moja ya mazungumzo yake amesema, kuna umuhimu wa kutekelezwa vilivyo mikataba iliyotiwa saini baina ya Iran na Kenya sambaba na kuondolea vizingiti katika ustawishaji uhusiano baina ya Tehran na Nairobi.

Ingia hapa chini kuangalia video ya mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran kama alivyohojiwa na Mubarak Henia.

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)