Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 13 Agosti 2014 17:01

Video ya Hamas inayoonesha jinsi ilivyoendesha operesheni kaskazini mwa Ghaza

Kitambulisho cha askari wa Kizayuni mwenye cheo cha Luteni wa Kwanza kikiwa mikononi mwa Hamas baada ya wanajeshi wa Israel kukimbia katika medani ya vita Kitambulisho cha askari wa Kizayuni mwenye cheo cha Luteni wa Kwanza kikiwa mikononi mwa Hamas baada ya wanajeshi wa Israel kukimbia katika medani ya vita

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesambaza mkanda wa video unaoonesha namna wanamapambano wa Izzuddin al Qassam, tawi la kijeshi la harakati hiyo lilivyoendesha operesheni zake kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza na kuangamiza wanajeshi wanaokaribia 20 wa Kizayuni.

Katika mkanda huo wa video, mwandishi wa televisheni ya al Aqsa anaonekana akiwahoji wanamapambano wa Palestina katika mstari wa mbele wa mapambano na kuelezea namna walivyowawekea mitego wanajeshi wa Israel na kuwaangamiza kwa mpigo.

Mkanda huo unaozungumza kwa lugha ya Kiarabu aidha unaonesha picha mbalimbali ya ngawira walizochukua wanamapambano wa Palestina ikiwa ni pamoja na silaha za Wazayuni na vitambulisho vyao kikiwemo kitambulisho ya mwanajeshi mmoja wa Kizayuni mwenye cheo cha Luteni wa Kwanza ambao waliviacha na kukimbia katika medani ya mapambano ili kunusuru maisha yao.

Kwa mujibu wa mkanda huo wa video, wanamapambano wa Palestina wamesema hiyo ni sehemu ndogo tu ya video na maelezo mengi mbalimbali ambayo wameahidi kuyatangaza katika siku za usoni na ambayo wakiyatangaza yatazidi kulifedhehesha jeshi la utawala wa Kizayuni ambalo linadai kuwa halishindiki.

Itakumbukwa kuwa siku chache zilizopita, Mkuu wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, Osama Hamdan alisema kwamba, harakati hiyo ina picha za video zinazoonyesha hasara kubwa ulizopata utawala wa Kizayuni tangu ulipoanzisha mashambulizi yake katika Ukanda wa Ghaza, tarehe 8 Julai.

Ingia hapa chini kuangalia video hiyo iliyoko katika lugha ya Kiarabu

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)