Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 30 Julai 2014 11:31

Operesheni ya aina yake ya HAMAS imeangamiza wanajeshi kadhaa wa Kizayuni + Video

Operesheni ya aina yake ya HAMAS imeangamiza wanajeshi kadhaa wa Kizayuni + Video

Kanali ya Pili ya televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeutaka utawala huo ufanye uchunguzi kuhusu vipi wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina wamefanikiwa kufanya operesheni ya aina yake iliyoangamiza wanajeshi kadhaa wa Kizayuni kwa mpigo.

Televisheni hiyo imetoa mwito huo baada ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kutoa mkanda wa video unaowaonesha wanamapambano wake wakiwaangamiza wanajeshi kadhaa wa Israel katika operesheni ya aina yake waliyoifanya katika kituo cha kijeshi ka Nahal OZ.

Israel imekiri kuwa wanajeshi wake watano wameangamizwa katika operesheni hiyo ambayo makomandoo wa Hamas katika operesheni iliyochukua muda mchache sana, walitumia njia za chini kwa chini karibu na mpaka wa Ghaza kushambulia kituo hicho cha jeshi la Israel licha ya kituo hicho kuwa na vifaa vya kisasa vya kijasusi.

Ingia hapa chini kuangalia mkanda huo wa video:

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)