Wanaharakati wa ukombozi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina wamesambaza mkanda wa video katika mitandao ya kijamii ambao ndani yake anaonekana mama wa Kipalestina akionyesha radiamali (reaction) yake baada ya kumuona mwanawe akiwa hai.
Mama huyo wa Kipalestina alipewa habari kuwa mwanawe ameuawa shahidi katika mashambulizi ya kikatili yanayoendelea kufanywa hivi sasa na wanajeshi wa Israel huko Ghaza, Palestina. Hata hivyo alipofika katika hospitali ya ash Sifaa, alikabidhiwa mwanawe akiwa hai.
Mama huyo alishindwa kuzuia furaha yake ya kuchupa mipaka. Alianza kumpapasa mwanawe mwilini kuona je yuko salama,na je ni yeye hasa, je hakuna unywele uliopungua kichwani...
Katika mkanda huo wa video, wanaonekana jamaa wa mama huyo wakijaribu kumtuliza mama huyo bila ya mafanikio.
Ingia hapa chini kuangalia video hiyo