Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 14 Julai 2014 14:49

Wanamapambano wa Palestina washukuru msaada wa Iran na Hizbullah + Video

Wanamapambano wa Palestina washukuru msaada wa Iran na Hizbullah + Video

Makamanda wa mstari wa mbele wa Saraya al Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul Islami ya Palestina wamesambaza mkanda wa video ambao ndani yake wanaishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na harakati ya Hizbullah ya Lebanon kwa kulisaidia kwa kila hali na hasa kwa silaha na fedha taifa la Palestina ili liweze kujihami mbele ya mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wanamapambano hao wa Kiislamu wa Palestina wanasema katika mkanda huo wa video kama tunavyowanukuu:
"Tunatoa shukrani zetu nyingi sana na dhati kwa watu wote waungwana na wenye fikra huru duniani, kutokana na kuunga mkono muqawama kwa silaha na fedha ambazo zimetuwezesha kubadilisha mlingano wa mapambano katika medani.
Tunatoa shukrani zenu maalumu kwa ndugu zetu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wakati Iran inapoisaidia Ghaza, huwa inafanya hivyo ili kutekeleza wajibu wake wa kibinadamu na kidini. Na sisi tunatoa tena shukrani zetu nyingi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msaada na uungaji mkono wake huo na Iran kamwe haiwezi kulitupa na kulitelekeza taifa madhulu la Palestina katika mapambano yake ya kuwalinda watu wake na ardhi yake.
Katika vita vinavyokuja tutatumia mbinu za kisasa kabisa na kali zaidi kulikoni tulizotumia hadi hivi sasa.
Vile vile hatuwezi kuwa wakosefu wa fadhila, hivyo baada ya Allah Azza Wajallah, tunawashukuru pia ndugu zetu wa Hizbullah - wanamuqawama wa kusini mwa Lebanon - na hususan Sayyid Hassan Nasrullah kwa uungaji mkono wao wa kifedha, kijeshi na kiroho na kimaanawi."
Ingia hapa chini kutazama video hiyo.

 

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)