Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 17 Machi 2014 11:26

Video inayoonesha gaidi wa Syria akikiri kuvunja misikiti ya Ahlu Sunna

Video inayoonesha gaidi wa Syria akikiri kuvunja misikiti ya Ahlu Sunna

Ingia chini ya habari hii kuona video inayomuonesha kijana wa Kitunisia ambaye hivi karibuni amerejea nchini Tunisia  akitokea Syria ambako alikuwa akipambana bega kwa bega na makundi ya kigaidi nchini humo.

Kijana huyo amesema kuwa moja ya majukumu yao nchini Syria lilikuwa ni kubomoa Misikiti ya Waislamu wa Madhehebu ya Ahlul Sunna na hasa misikiti iliyokuwa na majina ya makhalifa au Bibi Aysha, na kisha kulitupia lawama jeshi la Syria ya kuharibu misikiti hiyo.

Abu Qusway ameongeza kuwa, mkakati huo ulifanyika kwa shabaha ya kuwakasirisha wanajeshi hao ambao wengi wao ni Masuni ili wajitenge na serikali ya Syria. Ameongeza kuwa, wanawake waliopelekwa Syria kutoka nchi za Kaskazini mwa Afrika walikuwa na jukumu la kuwapiga risasi wanajeshi na raia kwa kuvizia.

Kijana huyo wa Tunisia ameiambia Televisheni ya al Mayadin kuwa, alichukua maamuzi ya kuwauwa wapiganaji wenzake ili aweze kurejea nchini Tunisia kwa uhuru kamili, kinyume cha hivyo asingeliweza kuruhusiwa kurudi. Kijana huyo amesema kuwa, nchi za Qatar, Saudi Arabia Uturuki na nchi nyingine za Magharibi zimekuwa zikitoa misaada ya kisilaha, kifedha na kilojistiki kwa makundi ya kigaidi nchini Syria.

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)