Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 27 Disemba 2015 16:24

Rouhani: Kuendelea vita Syria, Iraq ni kwa manufaa ya Israel

Rouhani: Kuendelea vita Syria, Iraq ni kwa manufaa ya Israel

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia udharura wa kuweko umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema kuwa, kuendelea vita katika nchi za Syria na Iraq si kwa manufaa ya yeyote ghairi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Rais Rouhani amesema hayo leo kwenye sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 29 wa Umoja wa Kiislamu hapa mjini Tehran na kuuliza swali akisema: Hivi kuidhoofisha Syria na Iraq ni kwa manufaa ya nani? Ameendelea kuhoji akisema: Je, kudhoofishwa Syria na Iraq ni kwa manufaa ya ulimwengu wa Kiislamu na majirani Waislamu wa nchi hizo? Je, kudhoofishwa Syria kutazinufaisha Uturuki, Jordan, Saudi Arabia, Qatar na Imarati au kunazidi kuifurahisha Israel tu?

Vile vile Rais wa Iran amekosoa vikali hatua ya baadhi ya nchi za Kiislamu za Mashariki ya Kati ya kutumia fedha nyingi kununua silaha na kubainisha kwamba, badala ya kununua silaha fedha hizo zinapaswa kutumika kwa ajili ya kutokomeza umasikini wa kimaada na kiutamaduni baina ya Waislamu.

Aidha ameyalaumu madola ya kibeberu duniani kwa kujaribu kuonesha kuwa Uislamu ni dini inayohimiza machafuko na vitendo vya kikatili na kusema kuwa, miongoni mwa majukumu makuu ya Waislamu leo hii ni kuutambulisha vilivyo Uislamu wa kweli kwa walimwengu.

Mkutano huo wa siku tatu unafanyika kwa mnasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na Wiki ya Umoja wa Kiislamu na unahudhuriwa na wageni zaidi ya 300 kutoka nchi 70 duniani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)