Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 27 Disemba 2015 11:18

Rouhani afungua mkutano wa Umoja wa Kiislamu

Rouhani afungua mkutano wa Umoja wa Kiislamu

Duru ya 29 ya mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu imeanza leo hapa mjini Tehran kwa hotuba ya Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa viongozi wa nchi za Kiislamu. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Rais Hassan Rouhani amekosoa vikali njama za madola makubwa duniani za kuionyesha dini ya Kiislamu kwamba, ni ya utumiaji mabavu.

Rais Rouhani amesisitiza kwamba, watu wote wanapaswa kushirikiana katika vita dhidi ya ugaidi na makundi yenye misimamo mikali.

Rais wa Iran amekosoa vikali pia hatua ya baadhi ya nchi za Kiislamu za Mashariki ya Kati ya kutumia fedha nyingi kununua silaha na kubainisha kwamba, badala ya kununua silaha fedha hizo zinapaswa kutumika kwa ajili ya kutokomeza umasikini wa kimaada na kiutamaduni baina ya Waislamu.

Rais wa Iran amesisitiza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Kiislamu kwamba, Waislamu hawana chaguo jingine ghairi ya Umoja wa Kiislamu na kwamba, kuna haja ya kuchagua njia sahihi ya kuelekea katika umoja.

Mkutano huo ambao unafanyika kwa mnasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na Wiki ya Umoja wa Kiislamu unahudhuriwa na wageni zaidi ya 300 kutoka nchi 70 duniani. Mkutano wa mwaka huu utajadili mada kuu ya "Migogoro ya Sasa Katika Ulimwengu wa Kiislamu".

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)