Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 26 Disemba 2015 15:56

Sh. Bakari wa TZ: Umoja wa Waislamu, suluhu ya changamoto zao

Sh. Bakari wa TZ: Umoja wa Waislamu, suluhu ya changamoto zao

Wiki ya Umoja wa Kiislamu ambayo huadhimishwa kati ya tarehe 12 na 17 Mfunguo Sita ama Rabiul Awwal  ilianza Alkhamisi iliyopita kwa maadhimisho ya Maulidi ya Mbora wa Viumbe Mtume Muhammad SAW katika nchi mbalimbali kote duniani. Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu. Kwa hivyo wiki hii ni fursa munasibu ya kukutana na kuchunguza udharura wa daima wa kuwepo umoja wa Kiislamu hasa katika kipindi hiki cha fitina na ghasia. Ili kujadili umuhimu wa Wiki ya Umoja wa Waislamu, tumezungumza na Sheikh Ahmad Bakari, Mkurugenzi wa shirika la Jenga Uislamu la Tanzania, ambaye anaanza kwa kuelezea sababu zinazoufanya ulimwengu wa Kiislamu ushindwe kutatua changamoto zinazoukabili kwa sasa....

 

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)