Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 26 Disemba 2015 10:22

'Mtume SAW ni mlinganiaji wa umoja wa Waislamu'

'Mtume SAW ni mlinganiaji wa umoja wa Waislamu'

Sheikh al Azhar wa Chuo Kikuu cha kidini cha al Azhar cha Misri amesema kuwa, Bwana Mtume Muhammad SAW ni mlinganiaji mkuu wa umoja na mshikamano baina ya Waislamu Duniani.

Shirika la habari la RASA limemnukuu Sheikh Ahmad at Tayyib akisema hayo jana wakati alipotoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa sherehe za Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na kusisitiza kuwa, siku ya kuzaliwa mtukufu huyo wa daraja ni rehema kwa viumbe wote na rehema za ujumbe wake zimevienea viumbe vyote duniani. Amesema ujumbe wa Bwana Mtume ni wa kujiweka mbali na mifarakano na upotofu, vita na mizozo na kuelekeza nguvu zote kwenye kuwaunganisha Waislamu na kuwafanya wawe na kauli moja.

Sheikh al Azhar vile vile amehimiza kufanyika juhudi za kweli za kukabiliana na fikra potofu na misimamo ya kuchupa mipaka.

Itakumbukwa kuwa, Wiki ya Umoja ambayo ni baina ya mwezi 12 na 17 Mfunguo Sita ilianza juzi Alkhamisi kwa maadhimisho ya Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW kwa mujibu wa baadhi ya riwaya.

Sherehe za Maulidi hufanyika kote duniani katika kipindi chote cha mwezi wa Mfunguo Sita na kwenye minasaba tofauti ya furaha ya Waislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)