Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 26 Disemba 2015 06:22

Ayatullah Araki: Adui hataki kuona umoja na mshikamano wa Waislamu

Ayatullah Araki: Adui hataki kuona umoja na mshikamano wa Waislamu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu za Kiislamu amesisitiza udharura wa kuwepo umoja na mshikamano kati ya Waislamu.

Ayatullah Muhsin Araki amesema kuwa, maadui wanalenga umoja wa mataifa ya Waislamu kwa kuanzisha makundi yenye mitazamo potofu na iliyofurutu mipaka. Ayatullah Araki ameashiria kwamba, maadui wanaelewa vyema mapenzi ya Wairani na Waislamu wa maeneo mengine ya dunia kwa dini ya Uislamu na kwa msingi huo wanatumia mbinu za aina mbalimbali kwa shabaha ya kuwaweka mbali na kuwatenganisha Waislamu na Mtume Muhammad (saw) na Qur'ani Tukufu.

Amesisitiza kuwa, maadui hao wameanzisha makundi vibaraka kati ya Waislamu wa madhehebu za Suni na Shia katika jitihada zao za kuchafua sura safi na inayong'ara ya Uislamu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, kundi la kigaidi la Daesh ni mfano wa wazi wa njama za maadui wa Uislamu na kuongeza kuwa, moja kati ya malengo ya maadui hao ni kuvuruga umoja na mshikamano wa nchi za Kiislamu kama inavyoshuhudiwa sasa huko Syria na Iraq.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)