Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 23 Disemba 2015 18:54

Rouhani: Qur'ani,Sunna ni nguzo za Umoja wa Kiislamu

Rouhani: Qur'ani,Sunna ni nguzo za Umoja wa Kiislamu

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Qur'ani Tukufu na Sunna ni nguzo mbili muhimu za Umoja wa Kiislamu duniani.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika kitongoji cha Rey kusini mwa Tehran alipokutana na wasomi wa eneo hilo. Rais Rouhani ameongeza kuwa sasa tunashuhudia namna madola makubwa duniani yalivyogonga mwamba katika kuikwekea Iran vikwazo vya kiuchumi. Ameendelea kusema kuwa katika kipindi cha miaka 12 iliyopita, maadui wameifanyia Iran dhulma kubwa kwa kupitisha maazimio dhidi ya nchi hii katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na pia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Akiashiria chaguzi mbili zijazo za Baraza la Wanazuoni Wanamchagua Kiongozi Muadhamu na Bunge, Rais Rouhani amesema wananchi wa Iran watajitokeza kwa wingi katika chaguzi hizo na kwa mara nyingine kuliletea fakhari taifa hili.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)