Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 25 Oktoba 2014 10:31

Uislamu Chaguo Langu (92)

Uislamu Chaguo Langu (92)

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala hii ambayo huwaaangazia watu ambao baada ya kufanya utafiti wa kina huamua kufuata njia ilyojaa nuru katika maisha ya dunia na akhera yaani Uislamu.
Katika makala yetu ya leo tutamuangazia kijana Muaustria aliyesilimu Lanzl. Karibuni kujiunga nasi hadi mwisho.
@@@
Sisi waanaadamu kwa dhati ya maumbile yetu asili huwa tunamuamini Mungu moja. Iwapo tutapuuza ukweli huu bado sauti kutoka ndani ya nafsi yetu itatuita kuelekea katika itikadi hiyo. La kusikitisha ni kuwa aghalabu ya matatizo tuliyonayo duniani yanatokana na kuwa wanaadamu wengi hawaitikii wito wa ndani kabisa ya nafasi zao na hivyo kughiriki katika masuala ya kimaanda na kusahau masuala ya kimaanawi. Huu ni ukweli ambao Bw. Lanz anaashiria na kusema hitajia la kuwa na imani kwa dini na hasa kumuamini Mwenyezi Mungu ni dharura katika maisha ya wanaadamu. Anaongeza kuwa hitajilia la umaanawi katika maisha ya mwanaadmau ni jambo lisilopingika. Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa maisha bila umaanawi ni chanzo cha kuangua roho ya mwanaadamu. Natija nzuri na maridadi kabisa ya dini kwa mwanaadmau ni imani ambayo humuwezesha kuishi maisha mazuri yenye saada, utulivu na ufanisi.
Mwanaadamu katika dhati yake anafuatilia saada na daima huwa ana wasi wasi kuhusu mustakabali wake huku akitaka kuwa na maisha bora zaidi ya aliyonayo katika siku za usoni. Kuwepo imani thabiti ya kidini ni jambo ambalo huondoa wasi wasi huu kwani itikadi ya kidini humfahamisha mwanaadamu kuwa dunia imeumbwa kwa malengo maalumu. Hii inamaanisha kuwa kila ambacho mwanaadmau anakitenda huwa na malipo na kwamba malipo ya watenda mema daima hayapotei. Imani hii humfanya mwanaadmau awe na matumaini kuhusu mustakabali wake.
La kusikitisha ni kuwa, utamaduni uliope katika zama zetu umepelekea kuondoka dhana nzuri kuhusu dini duniani hasa katika maeneo ambayo fikra za kimagharibi zimekita mizizi. Hivi sasa wanaadamu wengi wanaishi katika mzingira ambayo wanataka maisha ya anasa kamili ambapo wana itikadi potofu kuwa wakifa kila kitu kitamalizikia hapo. Fikra kama hizi ndizo ambazo zimepelekea umaanawi na dini kutokuwa na nafasi katika maisha yao.
Muaustria aliyesilimu Bw. Lanz anasema: " Chimbuko la tatizo la nchi za Magharibi ni watu kupuuza wito wa kimaumbile katika dhati ya nafsi zao kuhusu kuelekea katika kumuabudu Mungo Moja."
Bw. Lanz anasema alifika wakati katika maisha yake alipohisi utupu na kukosekana muelekea jambo ambalo limlimepelekea aanza kuutafuka ukweli ili aweze kuokoka. Ni katika harakati zake hizo ndio alipoweza kuujua Uislamu na kwa njia hiyo aliweza pia kuyajua mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Anafafanua zaidi kwa kusema: "Hakuna shaka kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa ni chimbuko la nuru ambayo ilienea kote duniani. Mimi namshukuru Mwenyezi Mungu sana kutokana na kuzaliwa katika zama ambazo nimeweza kuyajua na kuyadiriki Mapinduzi ya Kiislamu. Wimbi ambalo liliibuliwa na mapinduzi haya yalikuwa chanzo cha watu kuvutiwa na dini hasa Uislamu duniani."
Bw. Lanz anatoa tathmini yake kuhusu matatizo yaliyopo katika jamii za Kimagharibi kwa kusema: "Maisha ya kimaada na yaliyojaa anasa za kidunia ni maisha ambayo kamwe hayaweza kuridisha roho ya mwanaadamu. Mwanaadamu wa nchi za Magharibi au aliye na mielekeo ya Kimagharibi anaishi maishi ya kimashine ambayo yamemchosha. Ulimwengu wa Magharibi na wanaoufuata ni wagonjwa na tiba ya ugonjwa wao ni kuwa na imani ya kidini. Baadhi ya wanafikra wa Kimagharibi walionya kuhusu tatizo hili miaka mingi iliyopita lakini hakuna mtu aliyewatilia maanani. Natija ya hiyo ni kuenea na kukithiri ufisadi na maporomoko ya maadili katika jamii za Kimagharibi na hivyo kupelekea jamii hizo kuzoroota."
@@@
Hakuna shaka kuwa njia pekee ya kuokoka mwanaadamu ni kufuata imani ya kidini katika maisha. Hii ni kwa sababu dini inatutaka tuwe na maadili mema na tuwajibike mbele ya wanaadamu wenzetu sambamba na kutetea haki. Dini inatufunza kuwa kuna maisha ya keshi akhera baad aya maisha tuliyonayo duniani. Kimsingi ni kuwa dini inataka mwanaadmau aishi maisha bora ya binafsi na kijamii. La kusikitisha ni kuwa moja ya natija za ustawi wa kasi kiteknolojia katika kipindi cha karne moja iliyopita ni mwanaadamu kuwa mbali na umaanawi. Teknolojia imekuwa na manufaa kwa mwanaadamu lakini wakati huo huo kutokana na watu kufutrutu mipaka, pamoja na kuwepo ustawi wa kiteknolojia tumeshuhudia kuzorota na kudidimia maadili na umaanawi na natija ya hayo ni hasara kubwa kwa ustaarabu. Nchi za Magharibi zinazodai kuwa zimestaarabika sasa zimezama katika dimbi la kuabudu anasa na starehe jambo ambalo limemuondolea mwanaadamu utulivu wa kinafsi. Aghalabu ya wataalamu wa masuala ya kisaikolojia wanasema aghalabu ya maradhi ya kiakili walionayao watu wasiofuta dini ni maradhi yatokanayo na ukosefu wa imani imara. Ernest Renan mwandishi Muingereza wa kitabu cha 'Historia ya Dini' anaandika hivi: "Inawezekana ikkafika siku ambacho kila kitu tukipendacho kikaangamia na kile kilichokuwa kikitustarehesha zaidi kikaondoka duniani. Lakini ni jambo lisilowezekana kwa mvuto wa dini kuondoka bali daima mvuto huo utakuwepo."
Bw. Lanz anasema alipata mahaba na mapenzi ya Mwenyezi Mungu katika Uislamu. Kuhusu hili anasema: "Dini ya Kiislamu inaweza kukidhi mahitaji ya mwanaadamu katika kila nyanja. Uislamu unaenda sambamba na fitra na maumbile asilia ya mwanaadamu. Ni dini yenye mtazamo sahihi kumhusu mwanaadamu na ndio njia bora zaidi ya mwanaadamu kuwa na uhusiano wa kimaanawi na Muumba wake. Uislamu unakidhi mahitaji ya kiroho ya mwanaadamu. Kwa mtazamo wangu watu wa Austria sawa na Wamagharibi wengine wanahitajia sana muongozo wa kidini maishani kwani wanakumbwa na masaibu na matatizo mengi na njia pekee ya kufikia uokovu ni kuufuata Uislamu." Maustira huyu aliyesilimu anasema hivi sasa vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vinaenzea propaganda chafu hasa katika sekta ya utamaduni jambo ambalo ni hatari kubwa kwa vijana. Anaongeza kuwa Wamagharibi wanatumia mbinu zilizostawi katika sekta ya mawasiliano ili kuharibu akili za vijana. Anasema sekta za sinema, muziki na mambo yote yanayowavutia vijana hutumiwa kuwapotosha kiiutamaduni na hivyo kuwafanya wavutiwe na utamaduni wa kimagharibi hataka kama wenyewe hawataki. Lanz anaongozea kuwa: "Mimi ninaamini inawezekana kueneza Uislamu kwa kutumia sanaa ya sinema au muziki lakini kwa kuzingatia vigezo vya Kiislamu ili kuwa njia hiyo tuweza kuwaathiri vijana." Leo tunashuhudia ukitimia utabiri wa msomi Muingereza Bernard Shaw ambaye alisema kuwa utafika wakati ambapo Uislamu utaenea kote duniani. Leo watu wa Marekani na Ulaya wanasilimu kwa wingi na huo ni mfano wa kuwa sahihi utaburu wa Shaw. Katika moja ya vitabu vyake Shaw ambaye aliaga dunia mwaka 1950 alisema: " Imani ya Mohammad itakuwa imani ya mustakabali barani Ulaya.

 

 

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …