Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 14 Oktoba 2015 16:53

Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya katika Mwamko wa Imam Hussein AS

Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya katika Mwamko wa Imam Hussein AS

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika makala hii fupi ambayo inawadieni kwa mnasaba wa siku hizi kumi za mwanzo za Mwezi Mtukufu wa Muharram ambapo Waislamu na wapenda haki kote duniani wako katika majonzi wanapokumbuka tukio chungu la siku ya Ashura la kuuahwa shahidi Mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na wafuasi wake 72 katika jangwa la Karbala, Iraq ya leo. Tukio hilo la miaka 1375 iliyopita ni moja kati ya mapigano mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu. Chanzo cha kujiri tukio hilo hakikuwa ni kupigania maslahi binafsi ya mtu, kikundi cha watu au hata ya utaifa; lakini ukweli ni kwamba tukio la Karbala na kuuliwa shahidi Imam Hussein AS pamoja na wafuasi wake mashujaa ni madrasa ya mafunzo, malengo na ibra yakiwemo ya tauhidi, Uimamu, kuamurisha mema na kukataza maovu, kutetea haki, heshima ya nafsi, izza na kupambana na dhulma na mfano wa hayo kwa ajili ya wanadamu wote. Katika makala hii fupi tutaangazia lengo muhimu katika mwamako wa Imam Hussein AS nalo ni kuamurisha mema na kukataza mabaya.
Kuamurisha mema na kukataza maovu ilikuwa moja kati ya malengo muhimu zaidi ya mwamko wa Imam Hussein AS. Lakini suali ambalo linaulizwa hapa ni kuwa, je kwa kuzingatia sharti la kutekeleza wadhifa wa kuamurisha mema na kukataza mabaya linajumuisha pia kulinda maisha na mali, kwani nini basi Imam Hussein AS hakuzungatia sharti hili; na kuenda mbele zaidi na kutoa muhanga maisha yake na yake ya wafuasi wake sambamba na kukubali kuchukuliwa mateka Ahlul Bayt na mabinti zake? Katika kujibu swali hili tunapaswa kusema kuwa, iwapo mtu atafanya dhambi na maasia na katika hali ambayo kwa mtazamo wa kijamii na kisiasa yuko katika cheo cha juu ambapo kitendo chake kinaweza kuigwa na kuwa kigezo kwa wengine na anayoyafanya kuwa ni aina ya bidaa katika jamii; katika hali kama hii, kunyamaza Mwislamu yeyote, mwenye maarifa na aliyefungamana na imani yake, ni maasia na dhambi isiyoweza kusamehewa!
Katika upande wa pili tunapaswa pia kumzingatia na kuangalia sifa za mwenye kuamurisha mema na kukataza mabaya. Wale wenye jukumu kuu la risala na mafundisho ya Mwenyezi Mungu ni Mitume na waliotangalia katika dini pamoja na warithi wao. Hawa ni watu wenye majukumu maalumu mbele ya mafundisho na maamurisho ya Mwenyezi Mungu SWT.
Kwa hakika, iwapo kila Mtume angetekeleza maamurisho na majukumu yake kwa mujibu wa hali jumla iliyokuwepo pasina kujali, basi hakungejiri vita na uhasama baina ya mitume na maadui na wala maamurisho na mafundisho ya kidini pia hayangekuwa na athari yoyote miongoni mwa walengwa.
Wakati Nabii Ibrahim AS alipoanzisha mapambano dhidi ya wale wenye kuabudu masanamu alikabiliwa na wimbi kubwa la upinzani na uhasama kutoka watu na nguvuza kitwaghuti lakini pamoja na hayo alikuwa akivunja sanamu moja baada ya nyingine na hakuwa na woga wala wahka katika jukumu lake hili.
Nabii Yahya ambaye binafsi hakuwa na risala wala sheria lakini alikuwa mtetezi na mlinzi wa sheria zilizotangulia, na alikuwa amepata jukumu hilo moja kwa moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Katika kutekeleza jukumu lake hilo alikabiliana na kupambana na mataghuti wa zama zake. Aliendeleza mapambano yake na kusimama kidete hadi wakati pale alipouawa na kichwa chake kuwekwa mbele ya taghuti aliyekuwa ameamuru auawe.
Imam Hussein AS katika katika njia yake ya kuelekea Karbala, kila mahala au nyumba alimoshukia alikuwa anakumbusha kuhusu Yaha na namna alivyouawa na kusema: " Walikuwa hawayapi thamani mafundisho ya Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba kichwa cha Yahya Bin Zakaria walikikabidhi kama zawadi kwa mtenda zina miongoni mwa Bani Israil."

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …